Home Uncategorized Jose Mourinho mmeshamlaumu sana, lakini Woodward mnamuachaje?

Jose Mourinho mmeshamlaumu sana, lakini Woodward mnamuachaje?

9594
0
SHARE

Zikiwa zimebaki siku 10 kuelekea mwisho wa dirisha la usajili, hali sio nzuri kwenye mipango ya usajili ya klabu ya Manchester United.

Mourinho juzi kupitia mkutano wa waandishi wa habari alisisitiza kwamba aliomba usajili wa wachezaji 5 miezi kadhaa iliyopita – mabeki watatu, kiungo, na mshambuliaji. Lakini mpaka sasa amepata wachezaji wawili tu – ukimuondoa Grant aliyesajiliwa kwasababu Sam Johnstone kauzwa na Joel Pereira huenda akatolewa kwa mkopo. Kutokana na ufinyu wa muda uliobaki – Mourinho amesema angependa apate angalau wachezaji wengine wawili lakini haoni hilo likifanikiwa, hivyo huenda akapata mchezaji mmoja.

Kuna tetesi kwamba Harry Maguire mwenyewe tayari anajiandaa kujiunga na Manchster United lakini mlinzi wa timu ya taifa ya Colombia anayekipiga Barcelona Yerry Mina amewafollow United kwenye account yao ya Instagram hapo jana na kuna dalili anakwenda United, hii yote ni kutokana na presha Mou anayomuweka Woodward.

United walishika nafasi ya pili katika ligi dhidi ya wapinzani wao City ambao wameendelea kujiimarisha pamoja na kumaliza ligi wakiwaacha kwa pointi 19. :
Pamoja na kurithi kikosi imara zaidi ya United, Pep amesaini wachezaji 20 ndani ya miaka 2 iliyopita, Mourinho amesaini wachezaji 9 tu.

Pamoja na utajiri mkubwa ilionao kuvizidi vilabu vyote vya soka duniani, United wamekuwa na tatizo kwenye kufanya usajili chini Ed Woodward. David Moyes alisajili mchezaji mmoja wakati alipoachiwa timu – na alilalamika kwamba bodi ya United ilimuangusha kwenye usajili. Van Gaal pia alitoa malalamiko kuhusu bodi na Woodward kwenye usajili na sasa Mourinho.

Inaripotiwa Woodward hupenda kusajili wachezaji ambao kibiashara huiletea timu faida nje ya uwanja, wachezaji wenye majina kuvutia biashara ya matangazo, mauzo ya merchandises, nk. Hivyo mara kadhaa amekuwa akipishana na makocha kwenye suala la usajili. Lakini pia wenye timu – The Glazers – wameripotiwa kwamba wao kuwa na mlengo wa kuingiza fedha zaidi kuliko masuala ya mafanikio ya timu uwanjani.

Uwepo na Ferguson na David Gill kabla, ulikuwa unaifichia United madhaifu yake. Walikuwa wazuri zaidi kwenye majukumu yao na kuiweza kuiletea mafanikio timu pamoja kuwa na wachezaji kadhaa ambao hawakuwa wa daraja la juu.
Kuondoka kwao kwa pamoja kumeiacha ‘uchi’ United, huu ni mwaka 5 hawajawahi kutwaa EPL, wamecheza Champions mara 3 tu na nafasi juu waliyomaliza ni robo fainali.

Hadi sasa Manchester United wako bila wachezaji wao 17 ambao Mourinho anawahitaji, kati ya hao kuna wachezaji tisa ambao wako majeruhi lakini pia kuna wachezaji 8 ambao hawajarudi kambini wanaendelea na likizo ya baada ya kombe la dunia.

Inasemekana kwamba Woodward alimuambia Mourinho kuhusu Kylian Mbappe, Neymar na Gareth Bale lakini Mou akakataa biashara hiyo kwa kuwa anaiona imeelemea upande wa kibiashara zaidi na sio matakwa ya kocha.

Woodward ana wachezaji ambao anataka waje Manchester United(kwa ajili ya biashara), lakini Mourinho naye ana wachezaji wake ambao anaamininwataisaidia timu, na mvutano huu unadaiwa umefika pabaya, tunasubiri kuona wapi inaelekea filamu hii ya boss na kocha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here