Home Uncategorized Dauda transfers: Tetesi na habari mbalimbali za Usajili (Maguire,Ramsey…)

Dauda transfers: Tetesi na habari mbalimbali za Usajili (Maguire,Ramsey…)

7924
0
SHARE

KCB bank, ndiye mdhamini rasmi wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa mwaka 2018/19 kwa jumla ya dau la Tshs million 420,000,000 bila ya kodi.

Alcacer anahitajika England

Barcelona inatarajia kumpoteza mshambuliaji wake Pablo Alcacer kwa klabu Watford. Hata hivyo Leicester City wamekuwa wakimwinda kwa dau la €30 million (£26.7m/$35m) kwa Alcacer huku ikisemekana kuwa dau hilo limeshakubaliwa naBarca.

West Ham washikilia usajili wa Quina

West Ham wamewavimbia Barcelona wanaomuwania Domingos Quina ili kumpa mkataba mpya. Mchezaji huyo mwenye miaka miaka 18 amebakiza kandarasi ya mwaka mmoja tu. Barcelona inasemekana ipo tayari kutoa dau la £600,000 kwa ajili ya kupata huduma za winga huyo machachari. Baada ya Barcelona kumuona Quina aliyekuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya U-19 ya Ureno waliotwaa ubingwa wa ulaya wamemfuatilia kwa karibu zaidi kuona uwezekano wa kumnasa.

‘Lewandowski azidi kuvutana na Bayern’

Robert Lewandowski ameweka wazi kuwa anataka kwenda nje ya Bayern Munich. Lewandowski anataka kwenda Real Madrid. Hata hivyo Chelsea pia inamuwinda. Kocha mkuu wa Bayern Niko Kovac ametamka kuwa hawana mpango wa kumuuza straika huyo.
Wakala wa Lewandowski, Pini Zahavi bado ameshikilia msimao kwamba mteja wake hana furaha klabuni hapo na lazima aondoke.

Olivier Giroud anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi ya kicha tangu msimu wa 2012/2013

1. Olivier Giroud 29

2.Cristian Benteke 29

3. Romelu Lukaku 21

4. Harry Kane 16

5. Peter Crouch na Andy Carrol wote wana magoli 15

Pereira kutathmini hatma yake Man united

Kiungo wa Manchester United amegoma kuongelea maisha yake ya baadae na klabu hiyo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza klabu hiyo. Andreas Pereira anatarajia kuonana na wakala wake kujadili hatma yake kwa mujibu wa jarida la Manchester Evening News. Pereira alikuwa kwa mkopo Valencia, ambapo inamtaka kiungo huyo 22 kujiunga na klabu hiyo kwa dili la muda mrefu. Atakutana na wakala wake kule mjini Miami kujua hatma yake. United wanatarajia kucheza dhidi Real Madrid siku ya jumanne. Pereira ana matumaini ya kumshawishi Jose Mourinho kumpa nafasi ya kudumu ugani Old Trafford.

Chelsea yamnyatia Ramsey & Vecino

Chelsea wanamfuatilia kwa karibu sana kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey na mchezaji wa Inter Matias Vecino kama mahitaji yao makubwa zaidi kwa mujibu wa Daily Mirror. Ramsey amebakiza miezi 12 tu na Gunners.

Kocha wa Arsenal Unai Emery anajiandaa kumpatia unahodha kiungo Mesutu Ozil mara nyingi zaidi baada ya kuiongoza Arsenal kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Paris Saint German

Roma yatibua mipango ya Arsenal kwa Nzonzi

Mkurugenzi wa Roma Monchi amethibitisha kupeleka ofa kwa klabu ya Sevilla kupata wino wa Steven Nzonzi, kwa mujibu wa FootMercato.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa France alijiunga na Sevilla mwaka 2015 wakati Monchi akiwa mkurugenzi wa klabu hiyo. Bosi huyo anataka kumkutanisha tena Nzonzi katika uga wa Stadio Olimpico. Arsenal na Barcelona zinamuwinda sana kiungo huyo wa zamani wa Blackburn na Stoke.

Leicester yamsaka tena Gibson

Leicester wanatarajia kupeleka ofa kwa klabu ya Middlesbrough kwa ajili ya kumpata Ben Gibson, kwa mujibu wa Daily Mail. The Foxes wanataka kuimarisha kikosi chao kwa kumuwinda mchezaji huyo mwenye miaka 25 kwa kumrudisha tena pale King Power Stadium. Kikosi cha Claude Puel kinamhitaji Gibson ili kuongeza nguvu kutokana na taarifa kuwa Harry Maguire anaweza kusepa.

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 28, ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Westbrom Msimu uliopita, na Sturridge anataka kuendelea kubaki Liverpool, na mpenzi wake amesisitiza Sturridge bado anaipenda klabu hiyo ya Liverpool

Sevilla yammendea flopu wa Chelsea Bakayoko kwa mkopo.

Sevilla inatarajia kufanya makubaliano na klabu ya Chelsea kumpata mfaransa Tiemoue Bakayoko kwa mkopo, kwa mujibu wa Daily Mirror. Kiungo huyo amekumbana wakati mgumh hasa kutokana na kiwango chake cha kusuasua sana Stamford Bridge. Taarifa pia zinadai klabu ya AC Milan inamuwinda.

Maguire “Siwezi kulazimisha kwenda Manchester United”

Difenda wa Leicester City Harry Maguire anafuatiliwa kwa karibu sana na klabu Manchester United. Lakini beki huyo amesema haweza kulazimisha kwenda Old Trafford, kwa mujibu wa Mirror. Jose Mourinho yupo tayari kutoa kibunda cha £65 million ($85m) kumpata mlinzi huyo wa kimataifa wa England. Leicester wameshikilia msimamao wao kwamba hawana haja ya kumuuza Maguire na meneja wao Claude Puel amesisitiza kuwa mlinzi huyo na Kasper Schmeichel wana furaha klabuni hapo wala hawana haraka ya kuondoka. Hata hivyo Klabu ya Real Madrid imeingia kwenye vita ya kumnasa mlinzi huyo.

Giroud kupambana mpaka mwisho Chelsea

Olivier Giroud ana matumaini ya kubakia klabuni Chelsea licha ya kuhitajika Marseille, kwa mujibu wa Daily Mail. Kuna majina makubwa yametajwa kujiunga na Stamford Bridge, Gonzalo Higuain na Lewandowski lakini yeye amesema hana hofu yoyote.

Fosu-Mensah kubakia Man United

Timothy Fosu-Mensah amesema haoni sababu yeyote ya kuondoka Manchester United yupo tayari kupambania klabu hiyo kunyakua taji la Premier League.
Mlinzi huyo wa Netherlands/uholanzi pamoja na walinzi Axel Tuanzebe, Matteo Darmian na Eric Bailly ndio waliocheza kwenye kipigo cha mbwa koko cha 4-1 kutoka kwa Liverpool.

Klabu ya Napoli, imethibitisha kuwa inataka kumsajili beki wa pembeni wa klabu ya Manchester United, Matteo Darmian.

Darmian, ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuondoka katika klabu ya Manchester United, na kuhusishwa kujiunga na klabu za Inter Milan, na Juventus.

Usiache kufuatilia Dauda Tv Kitaa on fire. Shaffih Dauda (Instagram na facebook)

Privaldinho (Instagram)

# Shaffihdaudatransfers

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here