Home Kimataifa Vijana wa Tanzania wapata ushindi Norway

Vijana wa Tanzania wapata ushindi Norway

5865
0
SHARE

Timu ya vijana Magnet inayomilikiwa na kituo cha soka Magnet Youth Organisation cha Dar, leo imeshinda katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Norway Cup yaliyoanza leo jijini Oslo, Norway.

Magnet imepata ushindi magoli 2-0 ikiwa ni mechi yake ya kwanza katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu za vijana kutoka mataifabalimbali duniani.

Magnet imepeleka timu mbili kwenye mashindano hayo, timu ya kwanza ni ya vijana wenye umri wa miaka 13 na ya pili ni ya vijana wenye miaka 14. Jumla ya wachezaji 21 walisafiri siku ya Jumatano iliyopita kwenda Oslo Norway.

Michuano ya Norway Cup ndio michuano mikubwa  kwa vijana wenye umri 10 hadi 19, na michuano hii ipo tangu mwaka 1972 ambapo mwaka 2016 kulikuwa na timu 2199 katika michuano hii.

Ni mara ya kwanza kwa Magnet kushiriki michuano hiyo nchini Norway, vijana wana njaa ya kuwa mabingwa  wa mashindano hayo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here