Home Kitaifa Kocha amefafanua kilichombakiza Chuji Coastal Union

Kocha amefafanua kilichombakiza Chuji Coastal Union

8103
0
SHARE

Wakati watu kibao wakiamini uwezo wa Athumani Idd ‘Chuji’ umeisha kutokana na umri wake kuwa umekwenda kocha wa Coastal Union anasema bado anaamini Chuji ana uwezo ndio maana amembakiza kwenye kikosi chake cha msimu ujao.

Chuji ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia Coastal Union kupanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

“Mpaka Chuji amebaki, ujue kwamba anayo nafasi kwenye timu. Mchezaji veteran kama ni muhimu kutokana na kuwa mwalimu mzuri kwa vijana wanaochipukia na bado ana uwezo mzuri ndio maana nimembakiza”-Juma Mgunda, kocha Coastal Union.

“Kuna Casillas ambaye ni golikipa mzoefu katika nafasi yake, kupata golikipa mzoefu ni jambo jema kwa hiyo tuna kikosi kizuri kipo imara.”

Licha ya kuwa na wachezaji wazoefu kadhaa, Coastal Union ina wachezaji wengi vijana jambo ambalo kocha wa timu hiyo amesema falsafa yake ni timu kuwa na vijana wengi kwa sababu hata yeye alianza kucheza mpira wa ushindani akiwa na miaka 19.

“Ukipata vijana wenye miaka 19, 20, 21 wenye uwezo ukichanganya na wazoefu unaweza kufikia malengo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here