Home Kitaifa “Ilibidi Yanga wafungwe 7-0 kipindi cha kwanza”-Dylan Kerr

“Ilibidi Yanga wafungwe 7-0 kipindi cha kwanza”-Dylan Kerr

7181
0
SHARE

Yanga imechezea kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa Gor Mahia, mchezo wa kwanza ugenini Nairobi Yanga ilipigwa 4-0 mechi ya marudiano imefungwa 3-0.

Baada ya game kocha wa Gor Mahia Dylan Kerr amesema walitakiwa kuifunga Yanga magoli 7-0 katika kipindi cha kwanza lakini hawakutumia vizuri nafasi.

“Tulijua mchezo utakuwa mgumu lakini tungeweza kufunga hata magoli saba kipindi cha kwanza, lakini hatukuweza kufanya hivyo”-Dylan Kerr.

“Tulifunga goli dakika ya kwanza baada ya hapo hatukutumia vizuri nafasi lakini tukafunga goli la pili.”

“Wakati wa apumziko niliwaambia wachezaji wangu tunahitaji kufunga goli la tatu matokeo yawe 3-0 ili kuumaliza mchezo kwa sababu matokeo yakiendelea kuwa 2-0 wakipata goli(Yanga) watarudi mchezoni na kushinda.”

“Tukafunga goli la tatu kwa kutumia kona. Golikipa wetu Boniface Oluochi akafanya makosa (simlaumu) baada ya kupata presh kutoka Yanga.”

“Nimefurahi kushinda mchezo, pointi tatu ni faida kwetu mechi ijayo itakuwa dhidi ya Rayon Sports nyumbani Nairobi. Mechi hiyo itakuwa fursa kwetu kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali ya Caf Confederation Cup.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here