Home Ligi EPL Hivi nani anamshauri Mourinho? ameshakurupuka na anakwenda kukurupuka tena, HAELEWEKI!

Hivi nani anamshauri Mourinho? ameshakurupuka na anakwenda kukurupuka tena, HAELEWEKI!

19595
0
SHARE

Kuna muda kama mtu wa soka unaweza kukaa na kujiuliza hivi Mourinho anashauriwa? Na nani anamshauri? Na kama anamshauri je anamsikiliza kweli au anaamka tu na kukurupuka.

Unakumbuka mwaka 2014 Jose Mourinho alimkataa kabisa Romelu Lukaku? Pamoja na kumtoa kwa mkopo West Bromich na Everton alikofunga mabao 15 lakini bado Jose hakutaka kumkubali Lukaku, hakutaka arudi na akamuacha aende zake.

Miaka ikaenda baadae Lukaku akanza kuwa lulu Everton na baadaye akaja United wakakutana tena na safari hii akiwa kama nyota mkubwa sana duniani na akiwa kati ya washambuliaji wanoogopwa na mshambuliaji mwenye mabao mengi United ya Mourinho.

Rekodi za Lukaku tangu auzwe na Mourinho.

Mechi Magoli

2013/2014. 31 15

2014 – 2017. 110 53

Kelvin De Bruyne. Kelvin De Bruyne sio kweli kwamba ameng’ara akiwa na City lakini ukweli ni kwamba alichoongezeka City ni maturity katika soka ila uwezo wake ulikuwa mkubwa mda tu na haswa akiwa Wolfburg alionekana ana kipaji kikubwa kilichokataliwa na Mourinho.

Kama ulimuona De Bruyne aliyetoka Genk kwenda Chelsea alionekana ana uwezo kupiga pasi na kufanya maamuzi na alihitaji uzoefu tu ili kuwa bora zaidi, lakinu Mou alimoa mechi 3 tu za Epl akamuacha aende.

2013/2014 baada ya Mourinho kumuuza De Bruyne kwenda Wolfburg alianza kumuonesha Mou kwanini alifanya kosa kumuuza, baadaye anarudi EPL na ni kati ya nyota waliowakosesha United kombe msimu uliopita, akiisaidia City kubeba kombe.

Mo Salah. Kati ya vitu Salah alihojiwa ni kwanini alishindwa kuwa bora wakati akiwa Chelsea? Na alijibu kwa kusema anadhani hakuwa anaaaminiwa kama ilivyo sasa ila anaamini alikuwa na uwezo mkubwa.

Ni kweli, alikuwa Jose Mourinho ambaye aliruhusu Salah aondoke Chelsea kwenda Italia kwani hakuwa anaamini katika kipaji chake na sasa Salah naye amekuwa nyota bora duniani baada ya kutemwa na Mou.

Rekodi za Salah tangu ahamie Italia

Mechi Magoli

2015. 16 6

2015/2016. 34 14

2016/2017. 31 15

David Luiz.Mourinho alitoa ruhusa kwa David Luiz kujiunga na PSG mwaka 2014 kwa ada ya £50m, siku chache baada ya Luiz kuuzwa akakutana na kipigo cha bao 7 kutoka kwa Wajerumani akiwa anaitumikia Brazil.

Mou akaanza kuaminika kwamba huenda safari hii alifanya jambo jema kumuuza Luiz, HAIKUWA HIVYO kwani baada ya kiwango kikubwa cha Luiz ndani ya PSG akarudi tena Chelsea kwa ada ya £36m.

Kwa kusisitiza tu ni kwamba katika wachezaji watatu KDB, Lukaku na Mo Salah ambao waliwahi kuuzwa na Mourinho wamefunga mabao 77 kwenye msimu uliopita na usisahau hapo sijamtaja Leornado Bonucci na Juana Mata ambao nao ilikuwa hivi hivi.

Kwanini Martial anauzwa?

Habari iliyowaumiza vichwa Manchester United ni kusikia sikia Anthony Martial anauzwa, ukiwasikiliza mashabiki wengi wa Manchester United hili ni jambo ambalo hawataki kabisa kuliskia kwani nyota huyu ukiacha uwezo lakini ni kipenzi chao.

Martial anaonekana ni future ya Manchester United, ndio kwanza ana umri wa miaka 22 tu na anaonekana atacheza kwa muda mrefu zaidi kwani ana uwezo mkubwa mno kuliko nafasi anayopewa.

Rekodi za Martial vs washambulaiji wengine United.

Magoli. Dakika.

Romelu Lukaku 16 2869

Anthony Martial. 9 1582

Jesse Lingard. 8 1823

Marcus Rashford. 7 1806

Ukiangalia rekodi hizo utagundua ukiacha Lukaku anafuatia Martial kwa mabao mengi United, pamoja na dakika chache ambazo amekuwa akipewa lakini amewazidi mabao wenzake waliopewa muda mwingi.

Lakini sii hivyo tu ukija katika upande wa assists, Romelu Lukaku anazo 7 ndio anaongoza ila Rashford na Lingard wamecgeza dakika nyingi kuliko Martila ila Martial hapewi mda na anataka kuuzwa, kwanini anauzwa? Mimi sijui.

Martial sio habari, habari kubwa ni hii.

Manchester United na Wolves ziko katika maongezi juu ya mlinzi Marcos Rojo ambaye United wanataka £25m tu, United wanampunguza Rojo ili kutoa nafasi na pesa kwa Harry Maguire wanayemuwinda toka Leicester City.”

Sina akili kubwa ya soka kama Mourinho lakini kwa haihitaji akili kubwa ya soka kama ya wataalamu wa soka kama Shaffih Dauda ua Mourinho kuona kwamba hili ni kosa kubwa linaenda kufanyika.

Una Phil Jones, una Smalling, una Shaw, una Darmian wote hao huwaamini halafu leo unakuja kutaka kumuuza beki ambaye amekuwa kama killraka akicheza sehemu nyingi za eneo la ulinzi.

Manchester United hawana uhakika wa mabeki wao na kati ya wachache waliopo Rojo ni mmoja ya walinzi wanaowabeba beba na United wanamhitaji sana Rojo kwanu atlist anaonekana ana ubora kuliko wengine waliopo.

Kuna habari kwamba Mou ameanza kujaribu kumuweka Nemanja Matic katika sehemu ya mlinzi wa kati ili kuchukua nafasi kama Rojo akiondoka, kama Mou atamuuza Rojo na Martial halafu timu isipate matokeo sitashangaa kuona akiishia njiani msimu ujao.

Manchester United 1 Liverpool 4.

Binafasi nina wasiwasi sana na United ya msimu ujao, tangu kabla ya mchezo wa jana na hii ni kutokana na namna ambavyo Mourinho amekuwa akilalamika sana kuhusu maandalizi yao ya msimu ujao.

Kipigo cha asubuhi ya leo cha bao 4-1 toka kwa Liverpool inaweza kuwa salamu tosha kwa Mou na mashabiki zake kujiandaa kisaikolojia kwa kitakachotokea katika msimu unaofuata wa EPL.

Mbaya zaidi kinachokatisha tamaa ni Mourinho anayoongea kuhusu United kwa sasa, anaonekana kama mtu ambaye ameanza kukata tamaa kabla hata msimu mpya wa ligi haujaanza.

Jana baada ya kupigwa na Liverpool amekiri kwamba kwa uwezo wa United asingeweza kulipia hata kiingilio kuiangalia na akisikitika/kulalamika kuhusu ukosefu wa nyota wake katika timh hii.

Mou ni kama anawaambia United kwamba chochote kitakachotokea msimu ujao hiyo sio juu yake, tusubiri tuone.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here