Home Kitaifa Banda FC vs Manzese United: Derby yenye usaliti

Banda FC vs Manzese United: Derby yenye usaliti

8450
0
SHARE

Ni timu mbili zenye profile zinazofanana, timu zote ni mpya kabisa kwenye mashindano, zote zimeingia msimu huu.

Banda imeingia kwa kishindo kuanzia hatua ya awali ilikuwa imeshinda mechi zake zote kabla ya mechi yao ya #RoboFainali dhidi ya Burudani ambapo walitoka sare 1-1 ndani ya dakika 90. Changamoto ya mikwaju ya penati ikabidi itumike kuamua mshindi zikapigwa penati saba kila upande (zote zilifungwa) mshindi hakupatikana giza likaingia mechi ikaahirishwa.

Mechi ikarudiwa siku nyingine, dakika 90 tukashuhudia sare ya bila kufungana. Zikapigwa tena penati kuamua mshindi, Banda wakasonga mbele kwa ushindi wa penati 5-4.

Banda inatoka maeneo ya Mabibo-Loyola karibu na Kigogo, maeneo ya Mabibo Sokoni kulikuwa na Stim Tosha, Mpakani Kombaini na Mabibo Market timu zoote hizo zilikuwa na upinzani dhidi ya Banda lakini kwa sasa mashabiki wote wataungana kuipa nguvu Banda FC.

Manzese United ipo ukanda wa Misosi FC ambao tayari wametolewa kwa hiyo huenda mashabiki wa Misosi pia wakaamua kuwaunga mkono majirani zao wa Manzese.

Zinapokutana Manzese United na Banda FC zinatengeneza mechi inayogawanya pande pimbili za Morogoro Road katika wilaya ya Ubungo.

Hii derby ya Manzese United vs Banda FC inafanana kabisa na ile ya England Merseyside derby (Liverpool vs Everton). Sifa kubwa ya derby hii ni kwamba, kwenye familia moja unakuta imegawanyika kuna mashabiki wanaoiunga mkono timu moja wengine wanakuwa upande wa pili.

Inawezekana kuna shabiki anaishi Mabibo au Kigogo lakini mishemishe zake za kila siku zipo Manzese kwa hiyo anaamua kuliunga mkono chama lake la wana anaikacha timu ya nyumbani au mwingine anatoka Manzese lakini michongo yake ya hela ipo Mabibo leo anaamua kuwapa nguvu washkaji wanaokutana kwenye deals za kusaka mikwanja leo usaliti hauzuiliki.
#WastueWana tukunane uwanja wa #Kinesi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here