Home Kimataifa Nani anastahili kuwa mchezaji bora wa dunia kati ya hawa watatu? Tupige...

Nani anastahili kuwa mchezaji bora wa dunia kati ya hawa watatu? Tupige kura

19722
1
SHARE

Orodha ya wachezaji 10 bora wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA(Fifa Mens Player Award) ilishawekwa hadharabi na nyota hao 10 tayari wanajulikana.

Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Kylian Mbappe, Luca Modric, Antoine Griezman, Eden Hazard, Raphael Varane, Harry Kane, Kelvin De Bruyne na Mo Salah wanawania tuzo hiyo.

Lakini kati ya hao kuna wachezaji watatu ambao ndio wanazungumziwa zaidi katika tuzo hii, Cristiano Ronaldo, Kylian Mbappe na Luca Modric wanapewa nafasi.

Sasa kabla FIFA hawajatangaza mshindi wao mwezi wa tisa ni vyema sisi kama wasomaji wa shaffihdauda.co.tz tuanze kumjua mshindi wetu kabla FIFA hawajaleta wao, lakini kwanza tuwajadili.

1.Cristiano Ronaldo. Hata kama humshabikii lakini huwezi kataa Ronaldo anatisha na amefanya makubwa sana 2017/2018 kwa timu ya taifa lakini vile vile kwa klabu yake ya zamani Real Madrid.

Kwanza katika klabu hakuna ubishi kwamba kombe la Champions League lililetwa kwa nguvu kubwa ya Mreno huyu, kambani aliweka mabao 15 na Real Madrid wakabeba kombe mara ya 3 mfululizo.

Ukiachilia hilo lakini pia yeye ndiye mwenye rekodi ya mabao mengi Champions League 123 na ni mchezaji pekee aliyewahi kufunga mechi 11 mfululizo za Champions League.

Katika michuano ya kombe la dunia alifunga mabao 4 na kati ya hayo, mabao 3 (hattrick) alifunga katika mchezo mmoja dhidi ya Hispania na kuweka rekodi ya mchezaji mkongwe kuwahi kufunga hattrick.

2.Luca Modric. Watu hawamtazami sana labda kwa kuwa hana mabao mengi kumzidi Ronaldo lakini kuna wakati ambapo mchango wako kwenye timu ndio unakupa tuzo hata kama huna goli.

Mwaka 2006 kwa mfano Miroslav Klose alikuwa katika fomu kubwa akifunga mabao 5 kombe la dunia lakini tuzo ya mchezaji bora wa dunia ilienda kwa beki Fabio Cannavaro.

Modric hajabeba kombe la dunia na ana mabao 2 tu, lakini mchango wake kuipeleka Croatia fainali hizi ni mkubwa sana na mara zote alionekana mtu anayeibeba zaidi Croatia.

Katika mechi 5 alikuwa Man Of The Match mara 3(hakuna mchezaji aliyemzidi kwa hili) na ni mchezaji bora wa kombe la dunia lakini pia usisahau Modric ana Champions League nako pia alikuwa mhimili mkubwa hadi likapatikana.

3.Kylian Mbappe. Tumalizie na huyu, Mbappe ana kitu cha ziada lakini pia ana kitu anakosa tofauti haswa na Luka Modric achilia mbali Cristiano Ronaldo.

Mbappe ambacho anacho ni kombe kubwa zaidi ulimwenguni(kombe la dunia) na tena sio kuwa nalo tu bali mabao yake 4 yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kulipeleka kombe Paris.

Mbappe ameshinda kombe akiwa na miaka 19 anafanikiwa kufanya jambo hili kubwa ambalo wakongwe kama Messi na Ronaldo wanaonekana kushindwa kabisa kulifanya.

Amevunja rekodi ya Pele ya mwaka 1958 kufunga mabao 2 katika mechi moja ya kombe la dunia lakini vile vile Mbappe ameweka rekodi ya mchezaji mdogo kufunga katika kombe la dunia.

Mwisho, kwa mimi ukiniuliza ningepiga kura nadhani ningeiweka kwa Modric maana hata pasi zake Madrid zilichangia kiasi kikubwa kumuweka Ronaldo alipo na naona anastahili zaidi kuliko wengine.

Wewe unadhani nani anafaa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa sasa? Weka maoni yako hapa chini na kura tutahesabu hadi siku ya Jumanne nitatoa majibu.

Comments

comments

1 COMMENT

  1. Mim naona Messi anstahili zaid kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa muda mrefu kweny ngazi ya vilabu(kuwa mfungaji bora katika mashindano yote Ulaya) licha performance kweny wc haikuwa nzuri sana lakin kwangu mim namuona anasthili

Leave a Reply to swalha Cancel reply

Please enter your comment!
Please enter your name here