Home Kimataifa Mdomo wa #LeoTena utawaponza Kivule

Mdomo wa #LeoTena utawaponza Kivule

8499
0
SHARE

Leo Jumamosi July 28, 2018 inapigwa bonge la mechi #NusuFainali ya kwanza ya #NdondoCup2018 kati ya Faru Jeuri dhidi ya Kivule United kwenye uwanja wa Bandari, Temeke.

Katibu wa Faru Jeuri Abdallah Chapozo amesema kitakachowaponza Kivule leo ni mdomo wa #TeamLeoTena ambao wanawatupia maneno ya shombo.

“Tumejipanga vizuri kwa ajili ya #NusuFainali, Faru Jeuri ni timu kongwe kwenye haya mashindano lakini Kivule ni wageni kwa hiyo wana morali.

#LeoTena ndio wanawachongea Kivule kwa sababu wanaongea sana, Faru saizi yupo porini ametulia kwa sababu ya maandalizi na tunaamini #NusuFainali mapema kabisa ndani ya dakika 90 hatutamwacha mtu salama.

Kuna pori moja lipo Uzaramoni Kisarawe-Mwanelomango ndio ambako Faru ametulia. Heshima ya Faru inajulikana hata serikali inamlinda Faru kwa gharama kubwa kwa hiyo ni mnyama mkubwa ambaye anathamani kubwa.

Kivule watambue wanapambana na timu kubwa wasituchukulie kirahisi, nimefanikiwa kuwaona mara mbili kwa hiyo nimewasoma, nawahakikikishia wakazi wa Vingunguti, Buguruni, Kwamnyamani na Ilala kwa ujumla hatuta waangusha.

#FaruAplifaya tunashukuru kwa sapoti tunayoipata kutoka Amplifaya na wao hatuta waangusha.

Hatuwafikirii sana Kivule kwa sababu tumewahi kufika hatua kama hii, tunafikiria ubingwa wa #NdondoCup2018 iwe mara ya pili  kwenye mashindano haya. Mechi yetu na Kivule imeisha, mashabiki wetu wamezoea furaha na tutawafurahisha.

Nje ya uwanja kutakuwa na vita nyingine kati ya #TeamAmplifaya wakiongozwa na mtu wa nguvu Millard na Meena Ali ambao wako upande wa Faru Jeuri #FaruAmplifaya dhidi ya #TeamLeoTena chini ya Dahuu, Gea Habibu, Musa Hussein, Jose Mara wanaoisimamia Kivule United.
#NdondoCup2018 #WastueWana tukutane uwanja wa #Bandari

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here