Home Kimataifa Luiz Felipe Scolari apata kibarua kipya

Luiz Felipe Scolari apata kibarua kipya

8880
0
SHARE

Kocha Luiz Felipe Scolari, ameteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Palmeiras ya Brazil, kwa mara ya tatu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 69, amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ambayo ni bingwa mara tisa.

Scolari alianza kuiongoza Palmeiras kati ya mwaka 1997 na 2000, halafu alirudi kwenye klabu hiyo kwa zaidi ya miaka miwili mwaka 2010, baada ya Chelsea kumfukuza akiwa ana miezi nane kwenye kazi yake mwaka 2009

Akishinda Kombe la Dunia, akiwa na Brazil mwaka 2002

Scolari alirudi kuiongoza Brazil katika Kombe la Dunia ambalo lilifanyika nyumbani Brazil mwaka 2014, ambapo alifungwa na Ujerumani mabao 7-1

Kazi yake ya mwisho ilikuwa China akiiongoza Guangzhou Evergrade, na amekuwepo bila klabu tangu mwezi wa 11, 2017

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here