Home Uncategorized David Luiz afichua siri

David Luiz afichua siri

11677
0
SHARE

“Nilikuwa mchezaji wa akiba. Lakini kuna mchezo tulicheza huku tukiwa na changamoto ya walinzi wetu kupata majeraha hivyo timu ikawa inacheza ikiwa na upungufu wa walinzi. Lakini kocha hakubadilisha mfumo kisha niliamua kumfata na kumwambia anipe nafasi ili nicheze kama mlinzi” David Luiz

Nyota na mlinzi wa Chelsea, David Luiz Marinho ambaye msimu uliopita hakufanikiwa kupata nafasi ya kucheza huku sababu haswa ikitajwa kuwa ni majeraha aliyoyapata, hatimaye nyota huyo ameeleza asili yake katika maisha yake ya soka huku akifunguka kuhusu nafasi yake ya ulinzi huku akisema mwanzoni alikuwa akicheza kama mshambuliaji.

“timu yangu ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa ni klabu ya Sao Paulo kipindi nikiwa nna miaka 9, kisha nilipotimiza miaka 14 nikajiunga na klabu ya Vitoria Bahia”

“wakati nikiwa hapo tulishiriki michuano flani hukohuko nchini Brazil, safari ya kusafiri mpaka kufikia sehemu ilipokuwa ikichezwa michuano hiyo ilikuwa ni safari ya masaa 72. Nakumbuka kipindi iko nilikuwa nacheza namba 10 (kiungo mshambuliaji au mshambuliaji wa pili) na klabu yetu ilikuwa ikitumia mfumo wa 3-4-3, kama mfumo tulioutumia kipindi cha Kocha Antonio Conte”

“Alinikubalia. Niliingia nikawa nacheza kama mlinzi wa kati. Hatukufanya vizuri sana, tulimaliza kama washindi watatu lakini nami nilichaguliwa kama mlinzi bora wa mashindano” alisimulia nyota huyo raia wa Brazil.

Luiz amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Chelsea huku akishinda mataji kama ligi kuu Uingereza, klabu bingwa barani Ulaya, kombe la FA.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here