Home Kimataifa Watoto 21 kuiwakilisha Tanzania soka la vijana kimataifa

Watoto 21 kuiwakilisha Tanzania soka la vijana kimataifa

9212
0
SHARE

Magnet Youth Organisation ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linajihusisha na mafunzo ya mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto wa miaka 5-17 jijini Dar es Salaam.

Wana timu mbili,  chini ya miaka 14 na chini ya miaka 13 ambazo zimesafiri Jumatano ya July 25, 2018 kwenda kushiriki michuano ya vijana nchini Norway katika jiji la Oslo.

Wachezaji waliosafiri ni wavulana 20 na msichana mmoja ambao waliondoka Jumatano lakini mashindano yataanza rasmi July 28 siku ya Jumamosi.

Wamekuwa wakiendesha mafunzo hayo Tanzania kwa muda wa miaka 4 sasa na wana vituo vitatu kwa ajili ya mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo vituo vipo Mjini (Posta), Mikocheni pamoja na Mbezi Beach.

Ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii nchini Norway na vijana wana njaa ya kushinda michuano hii na wana hamu kubwa sana hasa ukizingatia kwamba baadhi yao hii itakuwa mara ya kwanza kushiriki michuano nje ya Tanzania.

Michuano hii ya Norway Cup ndio michuano mikubwa  kwa vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19, na michuano hii ipo tangu mwaka 1972. Mwaka 2016 kulikuwa na timu 2199 katika michuano hii.

Ni faraja kwa vijana hawa kuhudhuria michuano hii na uzoefu watakaoupata nchini Norway itakuwa katika maisha yao na huu unaweza kuwa mwanzo mzuri kwa vipaji vyao, hii inaweza kufungua milango kwa wachezaji wengine wadogo hapo baadaye.

Uongozi wa Magnets umepambana sana kufanikisha safari hii na pia wanatoa shukrani kwa TFF, Wizara ya Habari, Utamani Sanaa na Michezo pamoja na ubalozi wa Norway kwa kulifanikisha hili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here