Home Kimataifa Roma wanataka wapewe Messi waisamehe Barcelona

Roma wanataka wapewe Messi waisamehe Barcelona

12496
0
SHARE

Mabingwa wa Hispania FC Barcelona siku ya Jumanne walitangaza kumsajili winga wa kibrazil Malcom kutoka Bordeaux kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya uhamisho wa €41m.

Usajili huo umekuja baada ya Bordeaux kumzuia kinda huyo wa miaka 21 kusajiliwa na miamba ya Italia AS Roma baada ya Barcelona kutupa ndoano dakika za mwisho siku ya Jumatatu kabla Roma haijamaliza biashara.

“FC Barcelona na Girondins de Bordeaux wamefikia makubaliano kuhusu uhamisho wa mchezaji Malcom Filipe Silva de Oliveira. Dili hilo limegharimu €41m”-Barcelona walithibitisha.

Mchezaji amesaini na klabu makubaliano ya kucheza kwa misimu mitano, hadi mwishoni mwa msimu wa 2022/23.


Malcom alikuwa anatarajiwa kuwasili Roma Jumatatu usiku kwa ajili ya vipimo vya afya siku ya Jumanne kabla ya kuungana na wachezaji wenzake siku inayofuata kwenye ziara ya pre-season nchini Marekani lakini dili hilo lilipigwa chini na klabu yake dakika ya mwisho.

Barcelona waliingilia kati dili hilo baada ya kushindwa kumsajili Willian kutoka Chelsea na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Italia Barcelona wakapanda dau zaidi ya Roma ambao walikuwa tayari kutoa €38m.


Inaelezwa Malcom alikuwa anatupiwa macho na vilabu kadhaa vya Ulaya pamoja na vya EPL (Arsenal na Tottenham).

Malcom alifunga magoli 12 kwenye michezo 35 ya ligi aliyoichezea Bordeaux msimu uliopita.

Kutokana na unyamaa ambao Barcelona wameifanyia Roma, mwenyekiti wa klabu hiyo ya Italia amesema hawezi kuwasamehe licha ya Barca kuomba msamaha.

“Barcelona walituomba msamaha, lakini sikukubali kuwasamehe. Njia pekee ya kukubali kuwasamehe ni pale watakapoamua kutupa Messi”-James Palotta, mwenyekiti wa AS Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here