Home Kimataifa Meneja amethibitisha Levante inamtaka Samatta

Meneja amethibitisha Levante inamtaka Samatta

16968
1
SHARE

Vyombo mbalimbali vya habari vya nchini Hispania vimeripoti kuhusu klabu ya Levante kumtaka Mbwana Samatta kwa ada ya uhamisho wenye thamani ya  euros (€)4m.

Mvutano kati ya vilabu hivyo viwili upo kwenye dau la uhamisho ambapo klabu ya Genk yenyewe inataka €8m ili imwachie Samatta kwenda kucheza ligi ya Hispania, La Liga.

Meneja wa Mbwana Samatta Jamal Kisongo amethibisha Levante kumtaka Mbwana Samatta a mazungumzo yanaendelea kuhusu dili hilo.

“Kweli Levante wameonesha nia na mazungumzo hayo yanafanyika kwa hiyo ni suala la muda tu tuone kama watakuwa wameafikiana.”

“Shida iliyopo ni kwamba, dau wanalodaka Genk Levante bado hawajafikia lakini kimsingi Levante wanamuhitaji sana Samatta.”

“Vipaumbele vya Samatta ni kucheza ligi ya Uingereza (EPL), Seria A ya Italia na ligi ya Hispania (La Liga). Ukiachana na Levante CSKA Moscow wanamtaka lakini yeye ana machaguo ambayo anaona ni sawa katika kutimiza ndoto zake.”

Kisongo amesema awali Genk walikuwa wanahitaji €12m lakini baadaye baada ya mazungumzo wakawa tayari kumuachia kwa €8m, lakini kwa €4m hadhani kama Genk wanaweza kukubali kumwachia.

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here