Home Ligi EPL Harry Maguire na mfupa uliowashinda Victor Lindelof na Dalley Blind Manchester United

Harry Maguire na mfupa uliowashinda Victor Lindelof na Dalley Blind Manchester United

11138
0
SHARE

Tetesi zimezagaa kwamba huenda mliniz wa Leicester Cuty Harry Maguire akajiunga na klabu ya Manchester United kama United watafanikiwa kukubaliana ada ya uhamisho na klabu ya Leicester City.

Wengi wamemfahamu Maguire kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha timu ya taifa ya Uingereza wakati wa kombe la dunia lakini Maguire alikuwa pia na msimu mzuri na Leicester City.

Kama hufahamu tu kati ya mambo ya kuvutia kuhusu Maguire ni kila timu anayochezea lazima awe mchezaji bora wa msimu, alipokuwa Sheffield alikuwa mchezaji bora wa msimu mara tatu.

Baadaye akauzwa kwenda Hull City lakinj waliposhuka daraja akaenda Leicester City ambako nako pamoja na Jamie Vardy kufunga mabao 20 ila Harry akaibuka mchezaji bora wa msimu wa Leicester.

Uimara wake. Harry ni mzuri sana katika mipira ya hewani, amekuwa imara sana kuokoa mipira ya kona na vile vile pale timu inaposhambulia amekuwa na msaada mkubwa kupiga vichwa.

Katika msimu uliopita Manchester United walikuwa wabovu kwa kufunga mabao yatokanayo na mipira ya kutenga, wakishika nafasi ya 12 EPL kwa kufunga mabao ya set piece.

Na hii inaweza kuwa faida kubwa kwa United kumuongeza mpiga vichwa mwingine atakayeungana na Romelu Lukaku kujariby kuruka wakati wa kona na faulu.

Jose Mourinho amekuwa akipenda sana wapiga vichwa, John Terry, Drogba unakumbuka walivyompa matokeo na huyu sasa anaweza pia kuwa aina hasa ya watu wake Jose.

Lakini pia anapokuwa na mpira amekuwa mtulivu sana na hii inamfanya kuwa moja ya walinzi ambao wanakuwa na uhakika wa pasi pale timu inapokuwa uwanjani.

Udhaifu wake. Harry ikipigwa counter attack utamkataaa, amekuwa na uwezo mdogo linapokuja suala la mashambulizi ya kushtukiza, wao wakishtukizwa au wanapotaka kushtukiza.

Hii inatokana na kutokuwa na speed ya kutosha na inampa wakati mgumu sana pale washambuliaji wenye kasi kubwa wakiwa wanakimbilia upande wake.

Wataalamu wanasemaje?Kocha wa zamani wa Uingereza Sam Allardayce anaamini anamuona Maguire akiwa mkubwa sana ndani ya United lakinu hili litatokana na kocha anayekwenda kuwa naye.

Sam amesisitiza kwamba ukienda United hupaswi kuwa lele mama na sio kwamba ukiwa bora katika klabu kama Leicester City baasi inamaanisha utakuwa bora United.

Pia Sam ameonya kuhusu aina ya kocha ambaye Maguire anakwenda kukutana naye, hajaweka wazi kuhusu Mourinho lakini amesisitiza kocha anaweza kumpoteza ama kumkuza.

Maguire hatakuwa beki wa kwanza kuonekana bora akiwa nje ya United na akakwama chini ya Mourinho kwani beki wa Sweden Victor Lindelof amekuwa aking’ara sana akiwa Sweden na wakati akiwa Benfica lakini akakwama akiwa na Jose Mourinho.

Dalley Blind naye alikuwa nyota akiwa Uholanzi akiwa na Ajax pia na baadaye kidoogo akaanza kuwa muhimu United ila Mourinho alipochukua timu akanza kupotea na sasa amerudi kwao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here