Home Kimataifa Yanayoendelea sokoni, United waivamia Leicester, namba 7 yamsubiri Hazard Real Madrid

Yanayoendelea sokoni, United waivamia Leicester, namba 7 yamsubiri Hazard Real Madrid

11992
0
SHARE

Manchester United wamganda Maguire. Hii inaonekana sio tetesi tena bali ni kweli Manchester United wametuma ofa ya kutaka kumsajili mlinzi wa kulia wa Leicester Cuty Harry Maguire.

Maguire alijiunga na klabu ya Leicester City msimu uliopita akitokea Hull City kwa ada ya £17m lakini sasa United wameambiwa watoe £66m kuweza kumnasa nyota huyo ambaye bado yuko mapumzikoni baada ya fainali za kombe la dunia.

Perez ageuka ruba kwa Hazard. Pamoja na vikwazo ambavyo Chelsea wanajariby kuweka ili Hazard asiondoke katika dirisha hili la usajili lakini unaambiwa raisi wa Real Madrid Florentino Perez hataki kuelewa.

Mwanzoni Chelsea ilisemekana wanataka £150m kama Madrid wakileta ombi la kumtaka Hazard lakini saaa inadaiwa Chelsea watahitahi si chini ya £170m kwa nyota huyo na Perez yuko tayari kutoa pesa hiyo.

Lakini hapo hapo Real Madrid inasemekana jezi namba 7 aliyokuwa akiivaa Cristiano Ronaldo imewekwa kando na anasubiriwa Eden Hazard kama mambo yakiwa sawa akaivae yeye.

Fujo za Liverpool sokoni hazijaisha. Tayari wana Allison Becker ambaye ni golikipa waliyemsaini kwa rekodi ya dunia ya kipa ghali kutoka As Roma, wamemnunua Xherdan Shaqiri, wana Fabinho wana Keita.

Lakini Liverpool baado wanaendelea kununua na sasa inasemekana wameshakubaliana na mlinzi wa Croatia/Bestikas Damogaj Vida na kinachosubiriwa ni kutoa £22m kwa Bestikas kumnunua nyota huyo.

PSG kuibomoa ngome ya ulinzi ya Bayern Munich. Kuna habari kutoka nchini Ufaransa kwamba klabu ya PSG imefikia sehemh nzuri kumpata mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng.

Bado mazungumzo yanaendelea kati ya timu hizo mbili na kama mambo yakiwa sawa tunaweza kumuona Boateng akiondoka Bayern Munich alikokaa kwa miaka takribani 7 sasa.

Martial anataka kuondoka ila hanunuliki. Kocha wa Manchester United Jose Mourinho inasemekana japo amemuacha Martial arudi Paris kumuangalia mpenzi wake Melanie Cru, anayetarajia kujifungua lakini Mou hajafurahi Martial kuondoka.

Uhusiano kati ya Mourinho na Martial sio mzuri na anaweza kumruhusu kuondoka, Chelsea na Bayern Munich wanaonekana kutaka saini yake lakini hakuna aliye tayari kutoa ada ya uhamisho ya Martial ambayo inakadiriwa kuwa £89m.

Sterling na Man City mmh!! Kuna habari za chinichini kutoka katika klabu ya Man City kuhusu mkataba mpya wa nyota wao wa Kiingereza Raheem Sterling ambao unaisha mwaka 2020.

Kwa sasa Raheem Sterling anapokea £170,000 na inadaiwa anataka apewe kiasi cha £250,000 na sasa City wanataka kuzungumza naye kuhusu hilo na kama hawatafikiwa muafaka baasi anaweza kuuzwa 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here