Home Kimataifa TBT, Drake na Rihanna usaliti wao sio chumbani bali hata uwanjani hawaeleweki

TBT, Drake na Rihanna usaliti wao sio chumbani bali hata uwanjani hawaeleweki

12318
0
SHARE

Leo ni Throw Back Thursday na si mbay nkurudishe nyuma katika couple za mastaa ambazo zimekuwa katika vyombo vya habari kwa muda mrefu ni hii ya Drake na Rihanna, mara nyingi wamekuwa wakirudiana huku sababu kubwa ikiwa ni usaliti.

Nilimuona Rihanna picha aliyopiga akiwa nchini Brazil 2014 wakati wa michuano ya kombe la dunia, alikuwa akiishangilia Brazil huku mlimbwende huyo akiwa na tattoo shingoni yenye bendera ya Brazil.


Mmmh baada ya michuano kwend na Rihanna kuisuport sana Brazil akaja akabadili gia baada ya Wabrazil kupigwa bao 7 na Ujerumani na hapo hapo akaanza kuwa shabiki wa Ujerumani katika michuano hiyo.


Mapenzi ya Rihana kwa Ujerumani yakawa maradufu kabisa baada ya Ujerumani kubeba kombe pale Brazil akaonekana kushangilia kombe lao na wachezaji wa Ujerumani huku akipewa jezi ya Ujerumani akaitema Brazil.

Lakini safari yake ya Urusi haieleweki maana alipoona Ujerumani wamerudishwa nyumbani alionekana kuwatosa na kuhamia upande wa Brazil ambao nao walipigwa chini.

Drake naye ni zaidi kuliko Rihana kwa sababu staa huyo wa nyimbo za kufoka foka anayesumbua chat za mziki na ulbum yake ya Scorpion ni shabiki wa karibu timu zote kubwa Epl.

Drake ni mshikaji wake sana John Terry na Drogba na wakati Terry akiwa Chelsea alikuwa akienda hadi mazoezi ya klabu hiyo kuangalia achilia mbali baadhi ya mechi alizohudhuria Stamford Bridge.

Lakini Drake huyu huyu ni mshikaji wa Le Bron James ambaye ni moja ya wawekezaji katika klabu ya Liverpool na hii inamfanya Drizy kuwaspoti majogoo na ameonekana na jezi ya klabu hiyo mara kadhaa.

Drake pia anaonekana ni mshabiki wa Manchester United na picha aliyopiga Carrington miaka kadhaa iliyopita alikuwa na jezi ya mashetani wekundu huku pia akiwa na jezi ya wapinzani wa United ambao ni Man City.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here