Home Kitaifa Mtwara waomba mwongozo waichangie Yanga

Mtwara waomba mwongozo waichangie Yanga

9944
0
SHARE

Kutokana na klabu ya Yanga kukabiliwa na hali ngumu ya kifedha huku baadhi ya viongozi wakitangaza kujiuzulu nafasi zao, wanachama wa klabu hiyo tawi la Mtwara wamesema wanatamani kuichangia timu yao lakini wanakosa mwongozo wapi wanatakiwa kuelekeza michango yao.

Katibu wa matawi ya Yanga mkoa wa Mtwara, Yusuf Mpame amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba mwongozo namna ya kuichangia klabu lakini hawapati ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi.

“Tuko tayari kutoa michango lakini tunaipelekeza wapi na katika utaratibu upi? Watu wa Mtwara tumeshawahi kuomba timu ije hapa angalau ifanye tour wakati wa pre-season halafu tuone tutafanya nini kwa ajili ya timu yetu, hatupatu hiyo nafasi.”

“Mambo mengi tumejaribu kuomba ushirikiano kutoka makao makuu lakini ushirikiano hatupati kwa hiyo sisi hata namna ya kutoa msaada tunashindwa kwa sababu hatujui tunapeleka wapi.”

“Tunaweza tukachanga lakini uongozi haupo karibu, upo kimya kutoa maelekezo. Tunaomba bodi ya wadhamini ituambie tufanyaje.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here