Home Kitaifa Makete yapaza sauti Sanga kutishiwa mapanga Yanga

Makete yapaza sauti Sanga kutishiwa mapanga Yanga

10089
0
SHARE

Baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga kujiuzulu na kutoa sababu kwamba, ameamua kufanya hivyo kutokana na kutishiwa maisha na baadhi ya wanachama wa Yanga waliopanga kwenda nyumbani kwake wakiwa na silaha za jadi kwa ajili ya kumfanyia fujo.

Chama cha Maendeleo Makete (MDA) kimekelaani kitendo cha baadhi ya wanajangwani kumtishia maisha aliyekuwa mwenyekiti wao ambaye pia ni mwenyekiti wa (MDA).

Uongozi wa Chama cha Maendeleo Makete (Makete Development Association- MDA) tumesikitishwa na taarifa kuwa  mwenyekiti wetu wa MDA Ndugu Clement Sanga ametishiwa usalama wake binafsi na familia yake hali hiyo ikihusishwa na majukumu yake katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa timu ya Yanga.

Akiwa kiongozi wetu katika MDA tunampa pole kwa yaliyotokea, nasi tunampongeza kwa uamuzi aliofanya wa kujiuzulu katika nafasi hiyo ya uongozi katika timu ya Yanga. Tunamtakia utulivu, subira na amani katika wakati huu wa mpito. Mungu amsimamie na kumzingira nyakati hizi.

Uongozi tunaungana na wanamakete na wadau wengine kumpa pole na kumpongeza kwa maamuzi haya aliyofanya akiwa salama yeye pamoja na familia yake.

Aidha tunampongeza kwa uongozi wake mahiri aliofanya kwa kipindi chote alichoiongoza Klabu ya Yanga kwa kuwa kulikuwa na utulivu na mafanikio makubwa kwa kipindi kirefu. Nasi tunaitakia klabu ya Yanga hali ya utulivu na subira katika wakati huu wa mpito ili ivuke na kuendelea salama.

Tunamuomba Bw. Clement Sanga tuendeleze mapambano ya kuwaleta wanamakete na wadau wengine wa maendeleo pmoja katika kuiletea maendeleo wilaya yetu.

ADV. PHILIPO MAHENGE, MAKAMU MWENYEKITI- MDA

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here