Home Kitaifa “Kuna wanaoachwa na kutolewa kwa mkopo”-Haji Manara

“Kuna wanaoachwa na kutolewa kwa mkopo”-Haji Manara

10936
0
SHARE

Kuelekea msimu ujao wa mashindano klabu ya Simba imepanga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji na kuwatema wengine.

Msemaji wa ‘Wekundu wa Msimbazi’ Haji Manara amethibitisha golikipa Said Mohammed ametolewa kwa mkopo japo hakutaja klabu anayokwenda.

“Said Mohammed ‘Nduda’ na baadhi ya wachezaji wengine wamepelekwa kwa mkopo kwenye timu tofauti-tofauti” 🗣Haji Manara.

“Wapo tutakaowatoa kwa mkopo na ambao tutaachana nao, lakini nadhani siku mbili hizi tutawataja wachezaji walioachwa na maandalizi yote kuelekea msimu ujao.”

Manara amesema hivi karibuni ataitisha mkutano na waandishi wa habari ili kutangaza wachezaji wanaotolewa kwa mkopo na timu wanazokwenda pamoja na wanaopewa mkono wa kwa heri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here