Home Ligi EPL Huyu ndiye “Melanie Cruz” mlimbwende matata aliyemuondoa Anthony Martial kambini

Huyu ndiye “Melanie Cruz” mlimbwende matata aliyemuondoa Anthony Martial kambini

16695
0
SHARE

Hali ya Jose Mourinho katika maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya Epl imezidi kuwa mbaya, baada ya Antonio Valencia kurudishwa nyumbani kutokana na majeruhi sasa Martial anadaiwa kulazimisha kuondoka kambini.

Inasemekana Anthony Martial aliomba ruhusa kwa Jose Mourinho kurudi nyumbani kwa ajili ya tukio la kuzaliwa kwa mwanae ambaye anatarajiwa kuzaliwa wakati wowote hivi sasa.

Chanzo cha habari kutoka kambi ya United nchini Marekani kinadai kwamba Jose Mourinho hakutaka Martial aondoke kwakuwa ndio mshambuliaji halisi aliyekuwa amebaki Marekani lakini mshambuliaji huyo alisisitiza kuondoka.

Melanie Da Cruz ndiye mrembo mpya wa Antony Martial, Melanie na Martial ni wapenzi kwa mwaka wa pili sasa na mara ya kwanza walikutana jijini Paris katikati ya mwaka 2016.

Melanie Da Cruz kiumri ni mkubwa kuliko Anthony Martial kwani amemzidi Martial miaka 4 lakini wazungu wanasema “age aint nothing but a number” na hili halikumzuia Martial kuwa naye.

Da Cruz aliwahi kushiriki Big Brother nchini Ufaransa na akaondolewa tu baada ya siku 72 huku mshindi wa shindano hilo alikuwa binamu wa kocha aliyepita wa Real Madrid Zinedine Zidane aitwaje Jonathan lakini kwa sasa ni mtangazaji katika Tv ya nchini Ufaransa.

Uhusiano wa wawili hawa ulikuwa motomoto zaidi baada ya Martial kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa mwanzo ambaye walizaa mtoto mmoja Samantha Jacquelint.

Kuanzia hapo Melanie amekuwa akionesha mapenzi ya waziwazi kwa baby wake huyo na kuanza kuvaa jezi za Manchester United mara nyingi akiwa kwenye mitoko yake ya kila siku mjini Paris.

Katika mitandao ya kijamii Melanie ni maarufu sana Ufaransa na watoto wa kiume wamekuwa washabiki wake wakubwa kutokana na aina ya picha ambazo amekuwa akipiga na ana followers milion 1.8 Instagram

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here