Home Kitaifa Coastal Union wamelamba dume

Coastal Union wamelamba dume

12769
0
SHARE

‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union ya Tanga imethibitisha kumalizana na mkali wa BongoFleva Ali Kiba ‘King Kiba’ kwa ajili ya kuicheza msimu ujao wa VPL na mashindano mengine.

Kwa Coastal United ni usajili mzuri, Ali Kiba ni mchezaji mzuri akuna shaka katika hilo kuna wachezaji wengi wanaocheza VPL nafasi moja na Kiba anaweza kushindana nao na akawa bora kuliko wao.

Baada ya mchezo wa hisani wa #TeamKiba vs #TeamSamatta, kocha Julio alisema, Ali Kiba ni mchezaji mzuri na ana uwezo kuliko wachezaji wengi wa ligi kuu Tanzania bara.

Julio alisema alishawahi kutaka kumsajili Kiba na kumwambia hana haja ya kwenda kuishi mkoni bali atakuwa anacheza mechi za Dar pekeake.

Mpira ni kitu ambacho Kiba anakipenda kutoka moyoni mwake na amesha weka wazi mara kadhaa. Tumemshuhudia akifanya mazoezi na akicheza mechi.

Amecheza Ndondo Cup, amecheza mashindano ya Ramadhani Cup pale JMK akiwa upande wa timu ya Bin Slum. Inawezekana kiwango alichoonesha kwenye mashundano hayo ndio kimepelekea kusajiliwa Coastal Union.

Mchambuzi wa michezo Geoff Lea kutoka Sports Xtra ya Clouds FM amesema Ali Kiba amewahi kumwambia kwamba kuna wakati alitaka kusajiliwa Azam FC.

“Aliwahi kuniambia kuna kipindi alitamani kusajiliwa Azam FC lakini connection hazikwenda sawa ili akafanye trio asajiliwe lakini alikuwa tayari na alikuwa anatafuta hiyo nafasi ya kusajiliwa”-Geoff Lea.

Inaonesha ni mtu ambaye yupo serious kwenye mchezo japo watu wanaweza kujiuliza kuhusu utimamu wake wa mwili. Kiba anafanya mazoezi ya mpira mara kwa mara kwa wanaomfahamu hawatobisha.

Coastal wamefanikiwa kibiashara kwa sababu haya mambo yanahurubiwa kila siku kuhusu vilabu kuwa na mlengo wa kibiashara, kama timu nyingine zimeshindwa kuleta value kwenye upande wa biashara Coastal Union wanawafundisha na wamefanikiwa.

Ni dhahiri kwamba, Ali Kiba ni miongoni mwa wasanii wakubwa nchini ambaye anafahamika kimataifa pia kwa hiyo umaarufu wake utaisaidia Coastal Union kibiashara.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here