Home breaking news Pata dondoo za yaliyojiri siku ya leo

Pata dondoo za yaliyojiri siku ya leo

9358
0
SHARE

Thiery Henry inabidi atafute klabu nyingne, maana wamiliki wa Aston villa wamesema Steve Bruce ataendelea kuwa kocha mkuu wa Klabu hiyo.

Singida United imemnasa kiungo wa Mwadui Fc AWESU ALLY AWESU “ZIGZAG” kwa kandarasi

Msimu Wa International Champions Cup-ICC 2018…

MICHUANO ya International Champions Cup (ICC) mwaka 2018, inatarajia kuendelea tena siku ya kesho Julai 26. Ambapo itapigwa michezo sita toka miji tofauti tofauti na majira nayo yatakuwa tofauti.

ICC CUP-MATCH DAY

★Juventus Vs Bayern Munich
Muda: 8:00 Usiku (Usiku wa kuamkia kesho)

★Borussia Dortmund Vs Benfica
Muda: 9:00 Usiku (Usiku wa kuamkia kesho)

★Manchester City Vs Liverpool
Muda: 9:00 Usiku (Usiku wa kuamkia kesho)

★Roma Vs Tottenham Hotspurs
Muda: 11:00 Alfajiri

★Ac Milan Vs Manchester United
Muda: 12:00 Asubuhi

★Atletico Madrid Vs Arsenal
Muda: 8:30 Mchana.

Bayern imempa mkataba mchezaji chipukizi mwenye miaka 17 Alphonso Davies kutoka katika klabu ta Vancouver Whitecaps kwa ada ya uhamisho ya $13.5m.

Real Madrid wanafikiria kumsajili Mshambuliaji wa Valencia, Rodrigo endapo Karim Benzema akiamua kuondoka. Kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui, anamhitaji, na alimfundisha Rodrigo wakati wawili hao wakiwa kwenye timu ya vijana chini ya umri ya miaka 21. Rodrigo akiwa Valencia tangu 2014, amecheza mechi 135, amefunga magoli 37

Akiwa timu ya taifa ya Hispania, amecheza mechi 9, na amefunga magoli mawili. Msimu uliopita wa 2017/2018, alifunga magoli 19 na kuisaidia timu yake ya Valencia kurudi kwenye ligi ya mabingwa ulaya (UL)

Klabu ya Fulham, imefanikiwa kumsajili mchezaji wa klabu ya Borrusia Dortmund, Andrei Schrulle, kwa mkataba wa miaka miwii.

Mtibwa Sugar imemalizana na Awadh Juma Issa aliyejiunga na klabu hiyo kwa miaka miwili. Issa ametokea klabu ya Mwadui FC

Brighto & Hove Albion inayoshiriki ligi kuu England, imemsajili mshambuliaji Alireza Jahanbakhsh kutoka Az Alkmaar, kwa dau la paundi milion 20. Nyota huyo wa timu ya taifa ya Iran, amesaini mkataba wa miaka mitano. Alireza, alifunga magoli 21, Msimu uliopita na amecheza mechi tatu za Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Iran

KLABU ya Lipuli kutoka mkoani Iringa imemsajili golikipa Abdallah Said Makangana a.k.a Dida aliyekuwa akiitumikia klabu ya Mtibwa Sugra ya mkoani Morogoro.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here