Home Kitaifa Mipango ya Kaimu Katibu Mkuu Yanga…”muda wa usajili bado upo”

Mipango ya Kaimu Katibu Mkuu Yanga…”muda wa usajili bado upo”

9862
0
SHARE

Baada ya kutangazwa kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Yanga, Omary Kaaya amezunguza na kuweka bayana mambo muhimu atakayoanza kuyatekeleza baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

“Kutokana na hali ya klabu yetu ilivyo inabidi kujitolea, ombi langu la kwanza kwa wanayanga ni kurudi kwenye umoja wetu, bila kurudi kwenye umoja, upendo na ushirikiano tuliokuwa nao mwanzo hatuwezi kujikwamua hapa tulipo na kusonga tunapopataka”-Omary Kaaya.

“Kwa hiyo rai yangu ni kuondoa ofauti zetu, kama kuna kambi au kutoelewana kwa namna moja au nyingine tuache hayo matatizo yetu turudi kwenye klabu yetu tuangalie jinsi gani ya kujikwamua kwa pamoja.”

“Tusaidiane na kushirikiana tutoke hapa tulipo, inawezekana kama tutafanya hivyo. Hilo ndio jukumu la kwanza.”

“Kurudisha hadhi ya klabu yetu kwa sababu tutakapokuwa wamoja na kujikwamua hapa basi tutaanza kutembea upya na kufika tunapotaka kufika na kurudisha hadhi ya klabu yetu.”

Dirisha la usajili kwa ajili ya wachezaji wa msimu ujao litafungwa kesho, Kaaya amesema muda bado upo na watafanya kila kinachowezekana ili kukamilisha nafasi zenye uhitaji.

“Kuna watu ambao walikuwa wanahuka na usajili na bado wanaendelea na hiyo kazi kwa muda uliobakia kumalizia maeneo muhimu kwa hiyo bado kuna muda huo uliobakia, tusubiri hadi dakika ya mwisho.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here