Home Ligi LA LIGA Tofauti ya Zidane na kocha mpya wa Madrid

Tofauti ya Zidane na kocha mpya wa Madrid

11274
0
SHARE

Real Madrid walimpa Lopetegui mapokezi mazuri licha ya mgogoro wake na uongozi wa timu ya taifa ya hispania.

Kila mwalimu ana mbinu zake. Kila mwalimu ana mazuri na mabaya yake. Na vyote hutumika ili kujua sifa za mwalimu husika.

Katika uwanja wa mazoezi wa Valdebebas, baadhi ya wachezaji wa Real Madrid wamefanikiwa kufanya mazoezi chini ya mwalimu mpya aliyechukua nafasi ya Zinedine Zidane, Julen Lopetegui. Tayari kuna tofauti zimekwisha anza kuonekana.

Kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kumeibuka baadhi ya mambo mawili.

Mawasiliano na mandalizi.

Zidane alikuwa akiwapokea wachezaji kwa hafla fupi kila mara wanapoanza kuingia kambini baada ya likizo ndefu. Kwa wakati huu hicho kitu hakipo.

Kocha wa viungo bwana Pintus alikuwa akichukua kikundi cha wachezaji kadha wa kadha na kuanza kuzunguka nao, kwenda juu kwemye majukuu ya uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu na kuwazungusha uwanja mzima wakitembea ikiwa kama sehemu ya mazoezi madogo ya kuandaa misuli. Kwa sasa hicho kitu katika mazoezi ya awali hakijaonekana.

Wakati wa mazoezi muda mwingi Zidane alipendelea wachezaji kutumia mpira zaidi, mazoezi ya nguvu kidogo, gym kidogo, mazoezi ya pumzi kidogo. Kwa sasa wachezaji wanatumia muda mwingi kwa ajili ya misuli yaan mazoezi ya viungo zaidi.

Lopetegui anatumia muda mwingi sana kuongea uwanjani, ni tofauti na Zidane ambaye yeye ni mkimya.

Wachezaji wengi wamekwishafika Valdebebas, ispokuwa Bale na Benzema,

Dani Ceballos, Theo, Borja Mayoral, Vallejo na Llorente wanaamfahamu kocha huyu zaiidi hivyo itakuwa rahisi kwao kumuelewa.

Sergio Ramos, Dani Carvajal, Isco, Marco Asensio, Lucas Vazquez na Nacho wanamfahamu sana Lopetegui na sidhani kama atakuwa mgeni kwao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here