Home Kitaifa Shaffih Dauda, Geoff Lea kuhusu uteuzi wa Omary Kaaya Yanga…’The hard way...

Shaffih Dauda, Geoff Lea kuhusu uteuzi wa Omary Kaaya Yanga…’The hard way is the only way’

11817
0
SHARE
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya (katikati) meneja wa Yanga Hafidh Saleh (kushoto) na Musa Kawambwa (kulia) mwandishi wa Azam TV

Siku moja baada ya kujiuzulu kwa makamu mwenyekiti wa Yanga, kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji na Bodi ya wadhamini, kimemteua na kumtangaza Omari Kaaya kuwa kaimu Katibu Mkuu katika kipindi cha mpito baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa kujiuzulu nafasi.

Kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Kaaya alikuwa afisa masoko wa Yanga.

Shaffih Dauda na Geoff Lea wamea mitazamo yao kuhusu uteuzi huo ambao umefanywa ili shughuli za kila siku za klabu ziende.

Shaffih Dauda

Wanachama waendelee na mambo yao wauache uongozi ufanye kazi, Kaaya amekuwa Yanga kwa muda mrefu kwa hiyo ni watu wa kuwapa moyo kwa sababu kwa namna mazingira yaliyo angekuwa mtu mwingine huenda asingekubali na kuamua kuendelea na mambo mengine.

Mara zote tunasema watu ambao wana passion na michezo na wapo kwenye nafasi kuongoza wanajua namna ya kukabiliana na hizi changamoto. Kaaya anapenda mpira na hayupo pale kwa ajili ya kutafuta kitu kwa namna ninavyomfahamu.

Wanayanga wampe ushirikiano kwa ajili ya kufanya kazi za klabu katika kipindi hiki wakati wanajipanga kurudi kwenye njia yao.

Geoff Lea

Kwa muda mrefu tumekuwa tuna lalamika kwamba vijana hawapewi nafasi hususan kwenye hizi timu kubwa, wakati mwingine sio lazima kupewa nafasi kwa mazuri, kuna wakati kwenye matatizo ndio unaweza ukamjua shujaa wa ukweli.

Kwa hiyo katika mazingira kama haya Kaaya hakuwa amewaza nafasi inaweza kujitokeza, inawezekana kichwani mwake alikuwa anawaza anaweza kufanya vitu vingi lakini nafasi haikuwahi kutokea lakini nafasi imetokea katika kipindi hiki ambacho tunaweza kusema The hard way is the only way ‘njia ngumu ndio njia pekee’

Katika mazingira magumu Kaaya amepata fursa ambayo watu wengi huwa wanaota kuipata lakini hawaamini kama wanaweza kuipata. Ni wakati wake kutuliza akili kwa sababu wanayanga kwa sasa sidhani kama kuna mtu yoyote anaipenda Yanga ataanza kupinga mtu filani hafai.

Anatakiwa kuthibitisha kwamba anatakiwa kuchukua nafasi hiyo kwa muda mrefu sio kwa dharura ambayo imejitokeza kwa muda huu mfupi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here