Home Kimataifa Real Madrid wajitathmini sana kwa Jr

Real Madrid wajitathmini sana kwa Jr

10803
0
SHARE

REAL MADRID

Real Madrid imemsajili Vinicius Junior kutoa Brazil. Kijana huyu fundi kila mtu anasema neno jema kwake. Wengine wanaamini kuwa huyu ndiye mchezaji pekee mwenye udambwi wa Neymar.

Mwandishi J. A. García wa gazeti la MARCA anamhurumia sana Vinicius. Anaamini kwamba hakustahili kuendelea kubakia hapo huku akitumika kwenye madaraja ya chini.

Vinicius akiwa na miaka 10 alijiunga na Flamengo; Alipofikisha miaka 13, akaitwa timu ya taifa ya vijana ya Brazil u-15. Alipofikisha umri wa miaka 16 na miezi miwili aliongoza U-17 katika michuano ya the South American Championship, alifanikiwa kuwa mfungaji bora na mchezaji bora wa michuano.

Dili lake lilikuwa vipi?

Tarehe 23 May 2017, akiwa na umri wa miaka 16, Vinícius aliuzwa na klabu ya Flamengo kwenda Real Madrid. Hakuweza kuitumikia Madrid kutokana na taratibu za uhamisho wa kimataifa wa mchezaji kutokuruhussu mchezaji wa umri wa chini ya miaka 18 kuuzwa nje ya taifa lake au kufanyishwa kazi nje ya taifa lake.

Mafanikio yake?

Mnamo mwezi June 2017, Vinicius aliwekwa nafasi ya 39 kama mchezaji bora duniani wa Umri wa chini ya 21 na jarida la The Telegraph. Wakati huo alikuwa mchezaji pekee anayetokea bara la Amerika kusini kuingia kwenye orodha hiyo.

Rekodi muhimu?
Dau lake la usajili la €46 million, lilimweka nafasi ya pili nyuma ya Neymar kama mchezaji ghali zaidi aliyeuzwa na klabu ya huko Brazil. Neymar aliuzwa Barcelona €86 million akitokea Santos licha ya kwamba taarifa zinadai kuwa Santos walipokea €17 million tu

Taatifa Binafsi
Majina kamili Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior
Tar Kuz 12 July 2000 ( 18)
Seh Kuz São Gonçalo, Brazil
Urefu 1.77 m (5 ft 10 in)
Nafasi Mshambuliaji

Vinicius anakwenda kucheza timu ambayo mchezaji aiyezaliwa nae mji mmoja Robinho aliwahi kucheza.

Kutambulishwa kwake Madrid!

Tarehe 20 Julai 2018, Madrid walimtambulisha rasmk Vinícius kama mchezaji wao halali mara baada ya kufikisha miaka 18.

Vinicius Junior atakuwepo msimu huu na Real Madrid 2018/19. Atacheza timu B, Castilla, na dakika kadhaa kwa timu ya wakubwa.

Shida iko wapi?

Changamoto kubwa ni kusikia mchezaji aliyetolewa milioni 45 anacheza Segunda B. Segunda B ni ligi daraja la 3 kule Hispania.

Je imewahi kutokea?

Alvaro Morata na Nacho waliunda sehemu ya kikosi cha Jose Mourinho msimu wa 2012/13, lakini pia walitumika kwenye kikosi cha Castila.

Msimu wa 2012/13, Morata na Nacho mambo yalikuwa hivi.

Morata alicheza mechi 18 (1,616 dakika) na Castilla na kufunga mabao 12, kwenye kikosi cha wakubwa alicheza mechi 15 (580 dakika) akafunga mabao mawili tu.

Nacho, alicheza mechi 19 (1,710 dakika) akiwa na timu B, chini ya Mou alicheza mechi 13 (863 dakika) lakini bado kiwango chake hakikuridhisha. Segunda sio sehemu sahihi ya kupima uwezo wa mchezaji ila unamdumaza tu.

Hata hivyo Castilla walikuwa ligi daraja la pili tofauti na sasa wapo daraja la 3. Ligi daraja la pili angalau pana kaushindani fulani lakini huko mchangani hakufai bora hata ligi daraja la kwanza anapocheza akina Farid Mussa hakufai,.

Mnamkumbuka yule Messi Martin Odegaard aliyesajiliwa na Madrid kwa mbwembwe kutoka Sweden? Yupo wapi? Na kipaji chake? Martin mwemyewe analalamikia viwanja vya Segunda B, hakuna ushindani ila mpira wa kule ni vurgu vurgu tu. Segunda B ni sawa na ligi yetu hapa bongo tu. Viwanja vibovu, hakuna hamasa.

Timu ya watoto
2005–2017 Flamengo
Timu ya wakubwa
Mwaka Timu M (G)
2017–2018 Flamengo 37 (7)
2018– Real Madrid 0 (0)
Timu ya taifa
2015–2016 Brazil U15 10 (7)
2016–2017 Brazil U17 19 (17)
2018– Brazil U20 0 (0)

Vinicius Junior anatarajia kucheza Segunda B ligi ambayo ni mbovu kuliko ligi ya Brazil aliyoikimbia. Anakwenda kucheza ligi ambayo mashabiki ni wapita njia, wapinzani wake wengi sio wacheza maprofeshno ila wahuni wahuni na watoto wa mitaani.

Sikuona sababu ya Julen Lopetegui kutokumjumuisha kwenye kikosi cha wakubwa. Mbona watu kama Mbappe, Martial na wemgineo walipata nafasi wakiwa na miaka 17 sembuse huyu mwenye miaka 18.

Kikos cha Castilla chini ya kocha Santiago Solari wamepewa mzigo mkubwa kuhakikisha mchezaji huyu anapata hamasa na kiwango chake kinakua licha ya kwamba wanashiriki mashindano dhaifu. Ni kama wamebebeshwa gunia la mayai

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here