Home Kimataifa Mbappe amemtema Messi kwenye Ballon d’Or, na kusema yeye ana nafasi ya...

Mbappe amemtema Messi kwenye Ballon d’Or, na kusema yeye ana nafasi ya kubeba

15378
0
SHARE

MBAPPE amemkataa MESSI nakumpa nafasi RONALDO kwemye kinyang’anyiro cha BALLON D’OR .

Nyota huyo wa Paris Saint-Germain amemtaja mshambuliaji mpya Juventus Ronaldo, mchezaji mwenzake wa ufaransa Raphael Varane, Luka Modric pamoja na yeye binafsi, kuwa wao pekee ndio wenye ubavu wa kupigania BDO.

Kylian Mbappe anaamini kuwa kazi aliyoifanya yeye inampa nafasi kubwa ya tuzo hiyo maarufu zaidi ya Ballon d’Or. Pia amewataja Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Raphael Varane kuwa wapinzani wake. Kinda huyo wa Paris Saint-Germain amesema haoni kama Lionel Messi ana ubavu wa kupambana kwenye tuzo za mwaka huu kutokana na klabu yake na timu ya taifa kufanya vibaya.

Mbappe mwenye 19 amekuwa akitajwa sana kama mmoja ya wachezaji watakaofanikiwa kutwaa tuzo hiyo ya dunia huku yeye mwenyewe akiamini kuwa ndoto hiyo huenda ikatimia mwaka 2018.

Kama Mbappe atafanikiwa kutwa tuzo hii basi atakuwa amevunja nazi iliyoshindika kwa miaka 10 kuwapoka tuzo Messi na Ronaldo.

Ronaldo aliyenunuliwa kwa dau la €100 million (£88m/$117m) na klabu ya Juventus yupo mbele hatua moja ya kuchukua tuzo hii huku akifuatiwa pia kwa karibu na mpinzani wake mkubwa kutoka klabu ya Barcelona.

Mbappe ameliambia jarida la France Football maneno hayo alipoulizwa kwa mtazamo wake yeye yupi anadhan anastahiki kutwa tuzo hiyos:

“kwa mtazamo wangu? aaaah naweza kusema , Cristiano Ronaldo, pia Luka Modric, hata Raphael Varane… aaah na mimi pia nastahili.”

Kinda huyo alisema mafanikio ya timu yake ya taifa na klabu yake yanampa imani kubwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye nafasi kubwa ya kutwa zawadi hiyo.

Mbappe amesifu sana kikosi cha timu ya taifa chini bwana Didier Deschamps:

“Bila unafiki mimi nilikuwa naamini tuna uwwzo mkubwa kabisa. wa kombe hilo. Kuna wakati nilisema hata kabla ya michuano kuanza kwamba hakuna wa kutuzuia sisi kufika fainali. Wengine wakaniona kama mwenda wazimu. Timu yetu ilikuwa na kila kitu. Nikawaambia tunakwenda kulichukua na kweli tumerudi nalo“

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here