Home Kimataifa Baada ya Cr7 kusaini Juve, sasa Messi naye ahitajika Serie A

Baada ya Cr7 kusaini Juve, sasa Messi naye ahitajika Serie A

9525
0
SHARE

Habari za usajili nchini Italia kwa mwezi huu ziligubikwa na Cristiano Ronaldo, usajili wake Juventus umekuwa gumzo kubwa sii tu kwa Serie A bali dunia nzima.

Lakini sasa wapinzani wakubwa wa Juventus timu ya Inter Milan imetajwa kutaka kujibu mapigo ya Juventus kwa kumleta mpinzani mkubwa wa Cr7.

Marco Tronchetti ambaye ni mkurugenzi wa Inter Milan amesema hakuna asiyemtaka Lionel Messi na kama ikatokea Inter wakapata nafasi kumnunua mchezaji huyo baasi hawatajiuliza mara mbili mbili.

Kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo, Messi naye anaonekana muda wake kucheza soka unaelekea ukingoni na hivyo kucheza soka nje ya Hispania inaweza kuwa jambo linalofuata kwake.

Lakini katika habari nyingine za usajili kutoka Serie A ni kwamba wakati Chelsea wakijiuliza uliza kuhusu kumnunua Gonzalo Higuain, Ac Milan nao wameingia katika mbio za kumnyaka mpasia nyavu huyu kutoka Juventus.

Inasemekana kwamba mlinda lango wa Ac Milan Gianluigi Donarruma anavutiwa na habari za yeye kuhitajika Chelsea na kama Courtois ataondoka Chelsea baasi angependa kuvaa gloves zake Stamford Bridge.

Wachezaji wa Juventus wamezidi kuwa lulu sokoni na sasa Daniele Rugani naye ametajwa kuwa mbioni kujiunga na Chelsea, lakini Juventus wamewaambia Chelsea kama wanamtaka watoe £44.6m.

Klabu ya Paris Saint German imewaambia Juventus, kama wanamtaka Angel Di Maria wanapaswa kutoa walau £50m na sii chini ya hapo, lajini sasa Juventus watakumbana na upinzani toka kwa Atletico Madrid kumnasa nyota huyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here