Home Kitaifa Sanga akimbia mapanga Yanga

Sanga akimbia mapanga Yanga

10719
0
SHARE

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake baada ya kupokea vitisho kutoka kwa mashabiki wamba watavamia nyumbani kwake kumfanyia fujo wakiwa na mapanga, majembe na mashoka.

Sanga amesema anajiuzulu nafasi hiyo kwa masikitiko kwa sababu ikuwa bado ana nafasi ya kuitumikia Yanga hadi mwaka 2020.

“Kilichonifanya nifikie uamuzi wa kujiuzulu ni baada ya utamaduni mpya ulioanza kujitokeza. Ijumaa iliyopita nimeona ‘clips’ mbalimbali zinatembea kwenye mitandao zipo nyingi za kubeza ambazo ni kawaida kwa sababu tumepewa dhamana ya kuongoza watu tofauti.”

“Shutuma zimeendelea hadi kuna clip inahamasisha kwa uwazi kabisa watu  mbalimbali kuja nyumbani kwangu na mapanga, majembe, mashoka, kwa ajili ya kunifanyia fujo.”

“Unaweza kupuuzia lakini hizi ndio tuhuma nzito maishani kwangu na mambo mengi mabaya huanza hivihivi.”

“Najiuzulu kwa masikitiko kwa sababu naamini nilikuwa ninakipindi kingine cha kuitumikia Yanga hadi 2020 kwa mujibu wa katiba yetu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here