Home Ligi EPL Klopp amechoshwa na ubahili

Klopp amechoshwa na ubahili

10524
0
SHARE

Liverpool wameamua kumwaga mahela kama Simba. Wanaaanza maisha mapya kwa sababu wamegundua maisha ya ubahili hayana tija.Neil Jones mwandishi wa tovuti ya goal.com ameainisha baadhi ya mambo muhimu kuhusu sajili za Lierpool.Kocha mkuu wa The Reds Bwana Jurgen Klopp alitanabaisha kuwa msimu uliopita hawana mpango wa kusajili. Nadhani msimu huu mabossi wa Liverpool matumbo.Baada ya mambo kwenda mrama Klopp anakiri kwamba anahitaji kushinda mataji lakini manunuzi ya miezi 7 iliyopita hayakukidhi mahitaji yake.Meneja huyu wa majogoo ya Liverpool amekuwa akisifika sana na mtindo wake wa kushambulia kwa kasi zaidi kuliko kujali mifumo ya kuzuia.Mfumo wake maarufu kama gegenpressing ulikuwa tishio sana msimu uliopita. Wazungu wenzake wanapenda kuita aina yake ya uchezaji kama ‘heavy metal football’ Anakwambia tufunge mawili tukufunge matano.Jurgen Klopp, msimu huu amegundua nini thamani ya ulinzi imara. Ujio wa Van Djik kwa mamilioni ya fedha ni dhahiri kwamba nae amegundu kuna haja ya kuweka milango imara hata kama mapazi yako ni bei mbaya.Huu ni miaka mitatu sasa tokea Mjerumani huyu kutua Mersey Tunnel. Hakuna alichowapa Liverpool zaidi ya medali mbili za ulaya (Uefa na Yuropa).Kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Klopp alijitangaza yeye ni ‘The Normal One’ akijaribu kukwepa ile mantiki ya Jose Mourinho ya kujiita Special one.Kila mshabiki anapenda kuona timu yake inamilili mpira wakati wot, lakini unapaswa kuwa na mipango kila mara, unapokuwa huna mpira na unapokuwa una mpira,” Klopp aliyasema hayo October 2015.Neil anasema hivi “Liverpool wapo “free” akimaanisha kwenye “creativity” akilenga ubunifu, yaani safu yao ua ushambuliaji imacheza kwa uhuru zaidi kila mchezaji akionesha uwezo wake. Lakini Liverpool hawana “stability” yaani sio Imara akijaribu kuamgalia jasa wakati wanapopoteza mpira. Hili ndilo suala linalomsumbua Klopp sokoni kwa sasa.Januari mwaka huu the Reds walivunja rekodi ya uhamisho kwa kutoa £75million ($98m) kumsajili Virgil van Dijk mlinzi wa Southampton. Miezo 6 baadae wameweka rekodi nyingine ya uhamisho kwa kutoa burungutu la takribani £66m ($86m) kumpata nyanda wa Roma mzaliwa wa Brazil Alisson Becker. Yote haya Klopp anajaribu kuongeza Stability kwenye ulinzi wao. Anajaribu kuingia kwenye mfumo ambao utamfamya acheze kwa kujiiamimi zaidi.Kumekuwa na ubutu katika safu ya kiungo cha kati. Liverpool wakajitoa kimasomaso kununua viungo wawili, mmoja raia wa wa Mali kwa dau la £90m ($117m) Naby Keita na Mbrazil Fabinho.Guardiola alipofika EPL msimu wa kwanza alovurugwa vyema. Maamuzi magumu ya Pep lutoa zaido ya Milioni 400 kiwekeza kwenye mabeki wemgi walimuona kama kavurugwa. Nadhani ametoa somo kwa wengine.Nadhani Klopp ameamua litafua maneno yake.Klopp mnamo July 2016, aliwananga Manchester United kwa kutoa hela nuingi kwa ajili kumpata Paul Pogba.“Kuna timu zinakwenda kutoa mafurushi ya hela ili kukusanya mastaa, unapomnunua mchezaji mmoja kwa £100m au zaidi halafu akapatwa na majeraha inakuwa kama umechezea noti ya hela kwenye jiko.“Mimi siwezi kufanya biashara hiyo. Hiyo hela lazima nifanyie mambo mengine, ikitokea siku nimetumia fedha nyingi kiasi hicho basi tiakuwa kocha wa soka kwa wakati huo.” Unadhani Mourinho anawaza nini kwa sasa? Bila shaka atakuwa na kicheko cha kinafiki kama ilovyo kawaida yake.Mwaka 2014 Chris Anderson na David Sally kwemye kitabu chao ‘The Numbers Game’ walikuja na mawazo kwamba kuzuia magoli kuna thamani kubwa zaidi kuliko kukimbilia kufunga mabao.Hapo zamani mabeki na walinzi wamekuwa wakidharaulika sana. Lakini Guardiola ametufungulia njia. Pia Klopp kupitia usajili wa Van Dijk na Alisson. Kwa mfano unadhani N’Golo Kante akitaka kuondoka Chelsea atanunuliwa kwa dau gani.Unadhani mashabiki wa Liverpool wamesahau lile tukio la usiku wa Champions League kule jijini Kiev?au kichapo cha mwaka 2016 kwenye fainali ya Europa League dhidi ya Sevilla. Lakini bado Neil anauliza vipi kuhusu beki wa kushoto? Kuna uwezekano wa Liverpool kutoa fedha nyingi? inawezekana kwa sababu watu kama Sandro wanauzwa bei za kununua visiwa.Ndani ya miezi 12 hii Klopp amebadilika sana. Anajaribu kuziba kila pembe ya Liverpool iliyoonekana kuna tatizo lolote. Ile tabia ya kuuza uza wachezaji hovyo wanagaka kuikomesha.Wamekuwa pia na kikosi kipana, Alberto Moreno anapishana na Andy Robertson, Alex Oxlade-Chamberlain ameletwa kuondoa changamoto ya kukosa wachezaji wazoefu. Fabinho na Keita wamekuja kuleta ushindani kwa Henderson na Wijnaldum, hata ujio wa Xherdan Shaqiri wa £13m unaleta tija na chachu kwemye safu ya ushambuliaji.Wamehofia kuanza msimu huku Loris Karius akiwa kipa wao namba 1. Neil hana ani kabisa na Simon Mignolet kwani tayari amekwisha ondoka kwemye kichwa cha Klopp. Imeandaliwa na kutafsiriwa na Privaldinho (Isntagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here