Home Ligi EPL Ubaguzi na siasa vyamng’oa Ozil timu ya taifa

Ubaguzi na siasa vyamng’oa Ozil timu ya taifa

9962
0
SHARE

Barua ndefu alioandika Mesut Ozil hii leo kwa mashabiki wake na timu ya taifa ya Ujerumani imehitimisha safari ya kiungo huyo wa Arsenal katika timu ya taifa huku sababu kubwa akitaja “Heshima”.

Ozil ameitumikia timu ya taifa ya Ujerumani tangu mwaka 2009 na sasa anasema kwa namna chama cha soka cha Ujerumani kinavyomchukulia hivi sasa hajisikii furaha kuvaa jezi ya timu ya taifa.

Chokochoko za Ozil na timu ya taifa zilianza baada ya mwanasoka huyo kupiga picha pamoja na raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye uhusiano wake na Ujerumani sio mzuri na hii ilizua kasheshe nchini Ujerumani.

Ozil na Tayyip walikutana mjini London n Ozil kumpa jezi ya Arsenal Tayyip jambo ambalo lilipelekea hadi meneja wa timu ya taifa Ujerumani Oliver Behorf kudai Ozil hastahili kuwepo katika timu ya taifa Ujerumani.

Ozil kuhusiana na tukio hilo amesema asingeweza kukataa mualiko wa raisi wa Uturuki ukizingatia kwamba yeye ana asili ya Uturuki na angekataa hata wazee wake wangekasirika.

Kinachomuumiza zaidi Ozil ni namna magazeti na vyombo vya habari nchini Ujerumani zinavyotumia picha hiyo kisiasa hali ambayo inamchafua kwani hakuwaza kabisa kuhusu siasa wakati anapiga picha hiyo.

Ozil ameonya kwamba mtu yeyote mwenye ubaguzi wa aina yoyote hapaswi kuongoza chama cha siasa kikubwa kama cha Ujerumani kwani mwisho wake ndio kunakuwa na matatizo kama yake.

Katika michezo 92 ambayo Ozil aliitumikia timu ya taifa alifanikiwa kufunga mabao 23 akatoa jumla ya assists 33 na alikuwepo wakati timu hiyo ikibeba kombe la dunia mwaka 2014.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here