Home Kimataifa Ndoto ya Kiemba kwa Himid imetimia

Ndoto ya Kiemba kwa Himid imetimia

11881
0
SHARE

October 2016 katika mishemishe zangu kwenye mitaa ya Shinyanga mjini nilikutana na Amri Kiemba miongoni mwa viungo bora kuwahi kuwashuhudia Bongo.

Kiemba alikuwa gym anajiweka fit kwa sababu wakati huo alikuwa anaitumikia Stan United ‘Chama la Wana’.

Katika story zetu za hapa na pale nikamuomba anitajie wachezaji watatu wanaomvutia kwenye soka la ndani.

Alichonijibu Kiemba ni kwamba, ana heshimu uwezo wa kila mchezaji kwa sababu kila mtu ana ‘strength na weaknesses’ lakini akasema anavutiwa na Himid Mao ‘Ninja’ kwa sababu anacheza mpira wa ushindani sana ambao hauwavutii mashabiki lakini unaleta matokeo.

“Mimi kama mchezaji namuelewa sana Himid Mao kwa sababu anacheza mpira wa kutafuta matokeo sio wa kuwapendeza mashabiki.”

Kiemba akaniambia katika vijana ambao anapenda awaone wanacheza nje ya nchi ni pamoja na Himid Mao kwa sababu ana moyo wa kushindana.

“Kwa hiyo katika vijana, ningependa Himid atoke Tanzania kwa sababu ana moyo wa kushindana kuliko kufurahisha mashabiki ambao ndio mpira wetu sisi.”

Kwa sasa huenda Kiemba anafuraha na amani kwa sababu alitamani kuona Himid anacheza nje ya Tanzania na jambo hilo limefanikiwa, hivi karibuni ‘Ninja’ alisaini mkataba wa miaka mitatu na Petrojet ya Misri.

Aliwataja pia Haruna Moshi Boban na Athumani Idd Chuji kama wachezaji bora wa kizazi chao.
#Ligend

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here