Home Kimataifa Liverpool walivyo na njaa kuonesha ujogoo wao msimu ujao

Liverpool walivyo na njaa kuonesha ujogoo wao msimu ujao

11874
0
SHARE

Jurgen Klopp anaonekana kuanza kuchoshwa nankuburuzwa na vigogo EPL na sasa wameamua kindaki ndaki kuanza kupambana na miamba mikubwa ya soka barani Ulaya.

Manunuzi ya mlinda lango wa As Roma Allison Becker kwa rekodi ya dunia ya mlinda lango inaweza kuwa salamu tosha kwa wapinzani namna ambavyo Liverpool wamemua kuspend.

Klopp amenukuliwa siku za karibuni akisema kuanzia sasa Liverpool hawako tayari kuuza key players wao na wako tayari kupambana sokoni kufanya manunuzi ili kuleta ushindani barani Ulaya.

Toka pesa wa Kirusi na Waarabu wameingia katika soka, upinzani umebadilika EPL na Man City, Chelsea na United zimekuwa klabu ambazo zimekuwa bora zaidi na hii imekuwa ikichagizwa na matumizi makubwa ya pesa.

Lakini Liverpool wenyewe wamekuwa wakisua sua na kununua wacgezaji wa kawaida tangu 2011 walipoondokewa na Fernando Torres, ila sasa hali imebadilika na manunuzi makubwa yameanza Liverpool.

Mwaka 2011 mfano Liverpool walinunua wachezaji 9 kwa gharama ya £109.9m, 2012 wakanunua jumla ya wachezaji watano kwa £30.32m tu.

Lakini kuanzia mwezi January hadi hivi sasa tunavyoongea Liverpool wamevunja rekodi ya mlinzi ghali zaidi Virgil Van Djik £75m na wamevunja rekodi ya kipa ghali zaidi Allison Becker £65m. Tuone namna manunuzi na mauzo ya Liverpool yalivyokuwa tangu 2011 hadi sasa.

Mwaka 2011, mauzo £79.1m,manunuzi £109.95m.

Walionunuliwa Jordan Henderson, Charlie Adam, Stewart Downing, Jose Enrique, Sebastian Coates, Craig Bellamy, Jordon Ibe, Luis Suarez, Andy Carroll.

Waliouzwa Paul Konchesky, Thomas Ince, Nabil El Zhar, Daniel Ayala, Sotirios Kyrgiakos, Christian Poulson, Raul Miereles, David N’Gog, Ryan Babel, Fernando Torres

Mwaka 2012, mauzo £14.3m, manunuzi £30.32m.

Walionunuliwa Fabio Borini, Joe Allen, Oussama Assaidi, Daniel Sturridge, Philippe Coutinho.

Waliouzwa Fabio Aurelio, Dirk Kuyt, Maxi Rodriguez, Alberto Aquilani, Craig Bellamy, Charlie Adam, Joe Cole, Christian Doni.

2013 Mauzo £28.7m, manunuzi £65.3m.

Walionunuliwa Mamadou Sakho, Thiago Ilori, Iago Aspas, Luis Alberto, Simon Mignolet, Kolo Toure.

Waliouzwa Stewart Downing, Jay Spearing, Jonjo Shelvey, Andy Carroll.

2014 Mauzo £72.87m, manunuzi £116.5m.

Walionunuliwa Rickie Lambert, Emre Can, Adam Lallana, Lazar Markovic, Dejan Lovren, Divock Origi, Javer Manquillo, Alberto Moreno, Mario Balotelli.

Waliouzwa Luis Suarez, Conor Coady, Pepe Reina, Martin Kelly, Jack Robinson, Daniel Agger, Oussama Assaidi, Suso.

2015 Mauzo £88.5m, manunuzi £76.02m.

Walionunuliwa Christian Benteke, Roberto Firmino, Nathaniel Clyne, Joe Gomez, Allan Rodrigues, James Milner, Danny Ings. Adam Bogdan, Marko Grujic.

Waliouzwa Raheem Sterling, Fabio Borini, Iago Aspas, Rickie Lambert, Sebastian Coates, Glen Johnson, Steven Gerrard, Brad Jones, Javier Manquillo.

2016 Mauzo £86.5m, manunuzi £69m.

Walionunuliwa Joel Matip, Loris Karius, Sadio Mane, Alex Manninger, Ragnar Klavan, Georginio Wijnaldum.

Waliouzwa Joao Teixeira, Jerome Sinclair, Sergi Canos, Jordon Ibe, Martin Srktel, Joe Allen, Brad Smith, Christian Benteke, Luis Alberto, Mario Balotelli, Thiago Ilori.

2017 Mauzo £47.25m Manunuzi £88.9m.

Walionunuliwa Mohamed Salah – £39m, Alex Oxlade-Chamberlain – £35m, Andrew Robertson £8m, Tony Gallacher, Dom Solanke.

Waliouzwa Andre Wisdon, Lucas Leiva, Kevin Stewart, Mamadou Sakho, Alex Manninger, Cameron Brannagan

2018 Mauzo £145m Manunuzi £252.75m.

Walionunuliwa Virgil van Dijk – £75m,Alisson – £65m, Naby Keita £55m, Fabinho £44m, Xherdan Shaqiri £13.75m.

Waliouzwa Philippe Coutinho na Emre Can

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here