Home Ligi EPL Naby Keita aliitwa Gerard, akamhusudu Iniesta, akaitwa Deco na sasa yuko Anfield

Naby Keita aliitwa Gerard, akamhusudu Iniesta, akaitwa Deco na sasa yuko Anfield

10968
0
SHARE

Mungu anakupa kile unachokitafuta, hivyo ndivyo ilivyo kwa kiungo mpya wa Liverpoil Naby Keita. Safari ya Naby hadi Anfield haikuja hivi hivi bali ilianza na wazo baadae kalifanyia kazi na sasa limetimia.

Keita anasema wakati akiwa mtoto sana hakuwa anawaza sana kuja kufika Ulaya lakini baba yake alikuwa mshabiki wa Liverpool hii ikamfanya aanze kuvutiwa na klabu hii.

Alianza kuvaa jezi ya Liverpool wakati huo akiwa na miaka 11 tu na alipokuwa mtaani akicheza mpira alikuwa akijifananisha na Steven Gerard na kuanza kuiga kila kitu chake hadi nafasi aliyokuwa akicheza uwanjani.

Lakini Keita anasema pamoja na kwamba baba yake alikuwa akiipenda Liverpool lakini mzee huyo alikuwa akivutiwa na kiungo wa Ureno Deco na kuanza kumuita mwanaye Deco kama nickname.

Naby Keita ni nani?

Mzaliwa katika kitongoji cha Conkary miaka 23 iliyopita ambaye safari yake barani Ulaya ilianzi mwaka 2013 nchini Ufaransa katika klabu ya Fc Istres.

Msimu wa 2014-2016 Keita alifanikiwa kujiunga na Red Bull Salzburg ya Austria akiichezea mechi 59 na goli 17 kabla ya kujiunga na Rb Leizpg ambayo aliichezea michezo 58 akafunga mabao 14 na ndipo alipohamia Liverpool kwa ada ya £57m.

Jezi namba 8 vipi?

Kwanza Keita anasema baba yake wakati alipokuwa akicheza soka nchini Guinea alikuwa akivaa jezi namba 8 na hii ilimfanya Keita naye kuanza kupenda jezi ya baba yake(namba 8).

Lakini Keita anasema pia mchezaji anayemvutia kabisa kuliko wote ni Andres Iniesta na ndio mchezaji bora kwake kuwahi kumuona na hii pia ilimpelekea yeye kuvutiwa na jezi namba 8.

Keita anasema katika vitu ambavyo amejifunza kwa Iniesta ni namna ya kuwa mbunifu uwanjani bila kugongana gongana na kupitia Iniesta amefahamu sio lazima kutumia nguvu kupwa uwanjani.

Kadi nyekundu kila kukicha.

Kama haufahamu tu ni kwamba katikati ya mwezi wa tisa hadi October 25 mwaka Jana Naby Keita alipewa kadi nyekundu 3 katika mechi 7 za timu ya taifa na klabu.

Lakini mwenyewe amesisitiza kwamba kadi hizo mara nyingi anapewa bahati mbaya kwani waamuzi wamekuwa wakikuza kuhusu tackling zake tofauti na ukubwa wenyewe.

Anapakumbuka nyumbani?

Kati ya vitu ambavyo Naby hasahau akiwa anarudi nyumbani kwao ni mipira na viatu, sio kwa ajili ya familia yake,Hapana ni kwa ajili ya watoto wanaocheza mpira mtaani.

“Huwa nikirudi nyumbani nanunua viatu vingi iwezekanavyo kwa ajili ya watoto wa mtaani kwetu, na huwa ninawaambia haijalishi wewe ni maskini kiasi gani au una hali gani unachopaswa ni kupambania maisha” alimalizia Keita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here