Home Kimataifa Je mauzo ya jezi yanarudisha hela ya usajili?

Je mauzo ya jezi yanarudisha hela ya usajili?

18542
0
SHARE

Wakati Neymar anakwenda PSG kuna watu waliamimi ile fedha £198m itarudi kwa mauzo ya jezi.

Jake Cohen, ni wakili msomi wa muasuala ya soka ambaye amewahi kushiriki katika mikataba mbalimbali.

Jake Cohen mwandishi wa the Guardian alimuuliza je Neymar kuna uwezekano hela yake ikarudi kwa jezi. Akajibu hkuna uwezekano huo chini ya jua.

Jezi ni udhamini na sio biashara tegemezi ya klabu. Klabu inaingia ubia na kampuni ya kutengeneza jezi kisha wao wanawalipa malipo ya kabla.

Kwa mfano kila timu inapotoa leseni kwa mtengenezaji wa jezi kuna kiasi kinawekwa mezani ikiwa ni sehemu ya makabadhiano ya haki za utengenezaji wa jezi hizo.

Manchester United wanapokea £75 million kwa mwaka kutoka kwa Adidas,
Chelsea wanapokea £60 million kutoka kwa Nike,
Arsenal wanapata £30 million kutoka kwa Puma

Kisha kila timu inapata asilimia 10-15 kwenye mauzo ya kila jezi.

Kwa mfano kwenye mauzo ya kila jezi
Mwezi July 10th Ronaldo alisanini mkataba wake na Juventus, Kupitia jarida la The Guardian, kwa masaa 24 jezi 520,000 ziliuzwa zikiwa na jina la Ronaldo.

Ripoti za beIN Sports zinasema juventus waliuza jezi 850,000 kwa mwaka mzima 2016/2017. Mauzo hayo ya jezi kwa masaa 24 yaliipatia klabu kiasi cha $60 million. Lakini kumbuka kwamba Juventus wanapata kiasi cha 10-15 kwenye mauzo ya jezi hivyo Adidas ndio watakaofaidi zaidi. Juventus watapokea kitita cha $9.

Kuna watu wanadhani kwamba unaposajili mchezaji mkubwa kwa gharama kubwa basi mauzo ya jezi yake pekee yatarudisha hela yote aliyonunuliwa. kumbuka kuna watu tayati wana jezi hivyo wanakwenda kubadilisha majina na namba tu. Wapo wahuni mtaani wanauza jezi feki na bado timu inapata asilimia 10 tu ya mauzo ya jezi.

Wengine wanadhani kwamba eti kampuni zinaomba majina ya kampuni zao yatokee mbele ya jezi ili kujitangaza. Hapana. Haya makampuni yanafaidika kwa kuuza jezi. Adidas chini ya CEO Herbert Hainer wanatarajia kupata dili la £1.5 billion ndani ya miaka 10 huku wakiingia ubia wa £750 million na Manchester United.

Watu wengine wanauliza kwanini klabu isitemgeneze jezi wao wenyewe wakajipatia asilimia 100. Jibu ni rahisi timu inacheza mpira na sip kutengeneza jezi. Kutengeneza jezi unahitaji wasambazaji wakubwa dunia, unahitaji kuendesha viwanda vikubwa, unahitaji kuwekeza kwa gharama nyingi sana. Kuendesha kiwanda cha nguo dunia nzima unahitaji uwe na Meli kubwa za mizigo, uwe na wafanyakazi sio chini ya laki, uwe na uhakika wa kupata malighafi za kuanda jezi sio chini ya milioni moja kwa mwaka hivyo ni ngumu sana kwa klabu kuingia kwenye biashara hizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here