Home Kitaifa VPL yaipeleka Simba Uturuki

VPL yaipeleka Simba Uturuki

12316
0
SHARE

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema wachezaji pamoja na benchi la ufundi watasafiri kuelekea Uturuki kwa ajili ya pre-season kwa lengo la kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara.

“Siku ya Jumapili  alfajiri klabu ya Simba itasafiri kuelekea Uturuki kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza August 22, 2018. Ikiwa huko itakaa hadi August 5 kisha itarejea Dar kwa ajili ya tamasha la Simba Day”-🗣Haji Manara.

“Msafara wa wafu 35 (wachezaji wote na benchi la ufundi) utasafiri kwenda Uturuki, tukiwa huko tunatarajia kupata mechi za kirafiki kwa kadiri benchi la ufundi litakavyoona inafaa.”

“Matarajio yetu pre-season hiyo tunayokwenda kufanya Istanbul itatusaidia kwa wachezaji wapya na wazamani kupata muunganiko mzuri kabla ya ligi kuanza.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here