Home Kitaifa Manara kamkataa Yondani

Manara kamkataa Yondani

15464
2
SHARE

Haji Manara amekanusha tetesi za usajili wa beki Kelvin Yondani anayetajwa kukaribia kujiunga na Simba.

Manara amesema Yanga ndio wanatengeneza picha zima la kumhusisha Yondani kutakiwa na Simba ili watakapo malizana nae ionekane kwa mashabiki kwamba viongozi wamefanya kazi yaziada kumbakiza.

“Hiyo ni movie inatengenezwa kwa ajili ya kuwapoza mashabiki wa Yanga, ionekane kwamba Simba ilimtaka ili watakapomalizana nae ionekane walituzidi ujanja.”

“Sisi hatuna mpango wala hatukumuhitaji, jambo wabalitengeneza wenyewe wanajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe, hakuna ishu ya Yondani na Simba kabisa.”

Kuna picha ambayo imeesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Yondani na Kazimoto wakiwa pamoja ambapo watu wamekuwa wakiihusisha na usajili wa Yondani kuhamia Msimbazi lakini Manara amei-punch pia.

“Mwinyi Kazimoto anahusika vipi na usajili wa wachezaji wa Simba? Mwinyi sio kiongozi wa Simba hajui chochote kuhusu mambo ya usajili kama yeye ni rafiki yake binafsi lakini haihusiani na usimba. Urafiki binafsi ni jambo jingine na Simba ni jambo jingine.”

Comments

comments

2 COMMENTS

  1. Kama maneno ya Haji Manara ni ya kweli basiYondani na viongozi wake wote wapuuzi….Yaani tunapata aibu Nairobi nyie mko busy kutengeneza movie……Upuuuuuzi kabisaaaa

Leave a Reply to Mayeji wa Mayeji Cancel reply

Please enter your comment!
Please enter your name here