Home Ligi LA LIGA Madhaifu na ubora wa Hazard, Neymar na Mbappe kwenye kuziba pengo la...

Madhaifu na ubora wa Hazard, Neymar na Mbappe kwenye kuziba pengo la Ronaldo

16563
2
SHARE

Real Madrid wanahaha sana kujua nani anafaa kuvaa viatu vya Ronaldo. Wameondokewa na mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika ardhi ya Ureno. Atakumbukwa pale Bernabeu kuliko hata makombe ya UEFA waliobeba kwa kipindi cha hivi karibuni. Huwezi kusema kwamba kuna kitu Madrid inamdai Ronaldo.

Wapo wachezaji watatu ambao wamatajwa sana kurithi mikoba ya Ronaldo

WARITHI WA RONALDO
Hazard Mbappe Neymar
Miaka 27 19 26
Thamani €150m €190m €200m
Takwimu
Magoli 139 48 203
Asisti 128 33 128
Michezo 494 105 350

MIKATABA YA WADHAMINI NA MATANGAZO:

Ushawishi kwenye mitandao ya kijamii

Ukitazama kwenye ukurasa wake wa , Mbappe wa Twitter hapo awali alikuwa na wafuasi 1.4 wakaongezeka hadi 1.65 ndani ya masaa 72 baada tu ya kutwaa ubingwa wa dunia. Inaonesha wazi kwamba siku za karibuni atapata wafuasi wengi zaidi hivyo kuna uwezekano mkubwa akakua kibiashara. Neymar ana wafuasi Milioni 40. Hazard ana wafuasi milioni 5 tu kwa upande wa twitter. Instagram kwa Neymar watu milioni 100 wamemfuata huku Hazard akiwa na watu milioni 15, na Mbappe akifuatwa na watu milion 13.

Real Madrid ni timu ya kibiashara lakini pia ni timu ya mafanikio. Kwa upande wa Biashara Neymar ana jina kubwa katika mitandao ya kijamii jambo ambalo litavutia mashabiki wengi na madili mbalimbali ya kimkataba hivyo dau lake litakuwa zaidi kama atajiunga na timu hiyo.

Mikataba na udhamini

Dili la Mbappe la mwaka jana na Nike hajaweka wazi ingawa wagu wengi wanadai kuwa ni moja ha dili kubwa zaidi kwake. Hata hivyo Mbappe ana utajiri mkubwa kwani amewekeza kwenye magari ya kifahari kama Ferrari, Mercedes-Benz, Audi, BMW, na Range Rover. Gharama zote za magari ya Mbappe inakadiriwa kufikia $890,000. Baadhi ya taarifa zinasema kwamba kama mikataba mipya ya Mbappe itapanda hadi kufikia Euro milioni 26 kwa mwaka kwa upande wa udhamini na matangazo.

Umri Njia za Mapato
19 Mikataba ya soka
Salary Endorsements
$26 Million Hajaweka wazi
Mkazi Udhamini
Paris, France Nike
Hadhi Misaada
Hajaoa Premiers de Cordee

Neymar ana mikataba mikubwa kama Nike, Red Bull, Gillette, McDonalds na Beats by Dre. Alipokuwa Barcelona alikuwa na uwezo wa kwenda nyumbani na Dola Milioni 18 kwa mwaka kutokana na malipo ya mikataba yake. Anashikilia nafasi za juu. Neymar ni brand kubwa zaidi kibiashara.

Muda kiasi
Sekunde €1.16
Dakika €70
Saa €4,200
Siku €100,821
Wiki €707,692
Mwezi €3.07m
Mwaka €36.8m

Januari 2015 Hazard alisaini mkataba wa $16 million. Kiasi hiki cha pesa ni sawa na kile anachoppkea Neymar kupitia mikataba yake tu achilia mbali mshahara. Ni wazi Neymar amempiku sana Hazard kibiashara. Mkatabawa Hazard utaisha June 2020. Hazard ana baadhi ya mikataba na wachina, China’s Sina Sports pia ana mkataba na Topps for a new trading card line, na ule wa Lotus Bakeries watengenezaji wa Biscoff brand ya biscuits. Mkataba wake mkubwa zaid Nike.

2017-18 Twitter GPG Mak
Mikataba No
Hazard $5 M 85 5.4 M 0.2266 $1.47 B
Mbappe 1.6 M
Neymar $17 M 19 40.4 M 0.6063 $0.97 B

Maelekezo

GPG: Bonasi za Magoli kila baada ya mechi,

Twitter malipo ya mikataba ya matangazo.

MAK: Makadirio ya utajiri kutokna mikataba mengine, makato na mishahara.

Eden hazard amekuwa na wastani mzuri wa kukimbia na mpira katika bara la ulaya. Ameweka rekodi ya kuwa katika ile ordha ya wachezaji watano wanaofanga vizuri zaidi. Hazard ni mbunifu. anacheza mpira kazi. Ni mara chache unaweza kumuona akicheza kwa madoido. Ni mchezaji ambaye aina yake ya umiliki wa mpira ni sawa na wa Cristiano Ronaldo.

Tena kuna uwezekano Hazard akawa na wastani mzuri wa kutokupoteza mipira kuliko Ronaldo, Neymar na Mbappe. Katika mikimbio 119 aliyokimbia Hazaed msimu uliopita alikamilisha kwa asilimia 90 na kupoteza 28 tu. Ana wastani wa 6.3, Messi akiwa na 5.5 akifuatiwa na Douglas Costa mwenye 5.3.

Neymar ni mchezaji mwenye faida nyingi. Mwepesi wa kufanya maamuzi. Mjanja, na pia ana umakini Mbele ya goli. Ana ufundi ambayo unawafanya wanaomkaba kumhofia mara anapokuwa na mpira. Kuna uwezekano katika mipira 10 atakayopoteza mitano au sita ikawa faulo. Na katika hizo faulo huenda zikawa katia eneo la hatari na kusababisha madhara.

Fahari kubwa ya Mbappe ni kasi yake na nguvu. Pili ana uwezo mkubwa wa kufunga. Nadhani huyu aweza kuziba majukumu yote ya Bale hasa pale anapoumia. Mbappe anaweza kufanya kazi 2 uwanjani, kucheza kaama wimga na wakati huo huo kutumika kama mshambuliaji msaidizi wa mwisho.

Madhaifu yao.

Hazard sio mfungaji mzuri. Hazard ana muda na mtu uwanjani. Sio mhamasishaji mzuri sana ukilinganisha na Ronaldo. Hazard sio mfanya biashara mzuri ili kuvutia wateja wengi kama nilivyosema hapo awali. Ni kazo kidogo kuamini kwamba Hazard anaweza kuwa na madhara makubwa kwenye mechi kubwa kubwa. Sawa Hazard anaweza kuidnesha timu vyema lakini huna uhakika wa yeye kufunga mabao. Kama tunavyojua mechi muhimu tunahitaji mabao tu. Haya mengine tutamwachia Modric na Isco.

Neymar anakosa kila kitu anachopaswa kuwanacho mchezaji mkubwa na tegemezi. Hana nidhamu. Katika umri wa miaka 26 bado amevaa hadhi ya kijana wa miaka 18. Hajakua kiuanamichezo wala hana kariba ya kuwa legendi. Hawezi kusimama mwenyewe na akabeba mzigo wa timu mabegani mwake. Hawezi kucheza kwa kutumia misuli yake nikimaanisha kijikakamua kama mtoto wa kiume. Hana hadhi ya kuvaa suti kwenye sherehe za kikubwa. Moja ya mambo ambayo Neymar anakosa ni kwamba ana uwezo wa kukimbia na mpira mara 7.5 kwa kila mechi lakini wastani wake ni 62. Maana yake anapoteza mipira mingi.

Mbappe
Bado ni kijaana mdogo. Madrid wanahitaji mtu wa kuvaa viatu vya Ronaldo. Wasiwasi mkubwa kwangu ni kifua cha Mbappe. Sijui ataweza vipi kubeba majukumu hayo. Hana uzoefu mkubwa sana.

HITIMISHO

Kayi ya wachezani wote hao wote wama magasi kubwa kwenye kikosi cha Madrid. Wanamuhitaji kila mmoja kutokana na kuziba kila mwanya alioacha Ronaldo. Wamahitaji mchezaji anayejituma, Neymar hapana anachezea kipaji tu, Hazard ndio anajituma, Mbappe ndio anajituma lakini bado mapema kuijua rangi yake haswa.

Wanahitaji mchezaji anayewafaa kibiashara ili kusaidia mauzo ya jezi nk., Neymar bila shaka atafaa, Hazard sio kivile, na Mbappe amekwisha onesha dalili hizo.

Wanahitaji mfungaji mzuri. Wamafahamu wanaenda kupoteza mabao 50 kwa mwaka. Hawa wote wakiwa na umri huu bado hayupo mwenye dalili za mabao 50 kwa mwaka. Hazard hapana na wala sio mfungaji mzuri sana, Neymar anaweza kufunga lakini ana mambo mengi mno, Mbappe msimi wa kwanza Monaco alifunga mabao 26 bila shaka katika umri wa wa miaka 18 hayo ni mabao mengi mno hivyo huyu anafaa sana kuziba pengo la Ronaldo kwenye suala la ufungaji.

Wanahitaji mhamasishaji anatayesimama na kuheshimiwa na kila mchezaji Madrid. Asimame kama baba. Neymar hapo amekwisha feli. Sio kiongozi hata kidogo. Ana utoto mwingi. Hazard ameiongoza Ubelgiji vyema. Ni mchezaji ambaye ni mcheshi, anajua kuishi na wachezaji wenzake. Hana makundi.

Kuna video moja inasambaa inamuonesha Rudiger akimsihi Hazard asiondoke. Bila shaka Hazard anawafaa Madrid kama kiongozi. Umri unamruhusu na hulka yake inampa nafasi hiyo. Mbappe bado ni mdogo. Labda Madrid ya 2022.

Mwisho? Madrid wajitafakari je wanataka kuziba pengo la Ronaldo kuondoka yaani kuzoba nafasi ya jina lake au mrithi wake? Kama ni mrithi wake wasubiri miaka 50 ijayo labda huenda mbinguni wakatuletea Ronaldo mwingine. Kinyume cha hapo wawanunue wote hao watatu watakuwa wameziba pengo lake na sio mchezaji mmoja.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram.

Comments

comments

2 COMMENTS

  1. Nimekukubali uchambuzi wako uko vizuri sana broo,ila umeniacha hoi hapo kwenye miaka hamsini mungu atuletee ronaldo mwingine

  2. Madrid kafeli kitu kimoja kama kutomshawishi cr7 kisa umri wake,lakini yule jamaa alikua na muda mrefu wa kucheza madrid hasa namba 9 kutokana na umri alionao kwa kusubiri mipira ya toni kroos,modric au casemiro na wangefanikiwa lakn sasa wamemuuza either kwa kutaka au kutotaka bila kuwa na mbadala mwingine’sema na rais perez ana mambo mengi sana huenda hajui alichokifanya,parvinho nakupa muda subiri laliga ianze uene madrid akichezea na timu ndogo kama celta vigo nk sababu zitaingia uwanjani bila pressure ya ronaldo hayupo.naishia hapoComment:

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here