Home Kimataifa Kipre Tchetche ananukia VPL

Kipre Tchetche ananukia VPL

16714
0
SHARE

Kuna kila dalili za mshambuliaji wa zamani wa Azam FC Kipre Tchetche akarejea tena Azam Complex kuitumikia klabu hiyo kwenye ligi kuu Tanzania bara na mashindano mengine.

Boss wa Azam FC Yusuf Bakhresa ameonekana kwenye video fupi ya Instagram akiwa pamoja na nyota huyo ambaye kwa sasa anacheza Terengganu FC ya Malaysia.

Katika video hiyo Yusuf anaonekana akimuuliza Tchetche kuhusu kurejea Azam. “Umemuona Kipre? Nafikiri sasa anarejea Azam…”

Kipre akamjibu Yusuf: “Yeah…Hallo boys, mnaendeleaje? Tutaonana hivi karibuni.” (Tafsiri siyo rasmi).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here