Home Kimataifa Jinsi World Cup inavyoziingiza “chaka” klabu kubwa katika usajili

Jinsi World Cup inavyoziingiza “chaka” klabu kubwa katika usajili

19896
0
SHARE

Nasikia  Manchester United wanamtaka Harry Maguire, na nasikia mabosi wa Bayern Munich wanapigana vikumbo kwa Benjamin Pavard, na pia sijastaajabishwa na jina la Guillermo Ochoa kuwepo kwenye list ya makipa wanaotakiwa kuchukua nafasi ya Courtois kama akiondoka Chelsea.

Sitashangaa na Man City nao kusikia wanamtaka Shaffih Dauda kwa kuwa ninachoona sasa ni kwamba vilabu vikubwa vinapapatika na namna watu walivyoperform kombe la dunia na michuano ya mataifa Ulaya pia hahaha natania bwana.

Lakini sikia, mwaka 1992 kuna bwana mmoja anaitwa John Jensen alipiga bao moja matata sana wakati wa mchezo kati ya Dernmark na Ujerumani katika michuano ya Euro, goli alilofunga Jensen lilimshawishi kila mtu kumuangalia mara mbili mbili.

Arsenal hawakutaka kumuangalia mara mbili mbili walichofanya wao ni kumalizana nae fasta alete magoli hayo Highbury, lakini huwezi amini alipofika Gunners alicheza miaka minne akiwa na goli moja, yakamshinda akasepa.

Achana na 1992 huko mbali sana na wengi wenu vijana wa juzi hamkuwa mumezaliwa nakuleta hapoo kwa mzee Madiba mwaka 2010 michuano ya kombe la dunia ilipigwa hapo na Asamoah Gyan akawa moja ya habari kubwa sana.

Sahau tuta lake zidi ya Waruguay lakini mpira mwingi aliopiga uliwafanya Wazungu wa Sunderland kutoa £13m kumnunua, haikuchukua muda, kiwango duni kiliwalazimu Sunderland kumuuza baada ya mwaka.

Hivi wangapi walimuona Juan Cuardado alivyokuwa wa moto kombe la dunia lililopita achana na hili, kila mmoja akasema Lionel Messi mpya amekuja alipokwenda Chelsea akawa na kiwango kibovu sana mechi 13 bao 0 akapotea,

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson alisema moja kati ya vitu ambavyo huwa anaogopa sana kuvifanya ni kusajili mchezaji baada ya mashindano mafupi kama kombe la dunia na mataifa Euro kwani mara nyingi wachezaji wanakuwa wamejiandaa kushndana kupindi kifupi.

Mwaka 2014 pia kuna James Rodriguez, achana na sura yake inayowavutia wadada wengiblakini uwezo alioonesha Brazil ulimfanya Perez kufungua pochi na kummwagia minoti aende Bernabeu, akaboronga.

Hiyo hiyo 2014 unamkumbuka mlinda mlango ambaye alizungumziwa sana ukiacha Manuel Neur? hakuna ubishia jina la Guillermo Ochoa lilikuwa mdomoni mwa kila mpenda soka kutokana na uwezo wake.

Lakini kabla ya kombe la dunia Ochoa alimaliza nafasi ya mwisho ya ligi nchini Ufaransa akiwa na klabu ya Ajaccio, akawa na kiwango kibovu sana mechi za kujiandaa na kombe la dunia na watu wakaanza kumpinga lakini kombe la dunia lilipoanza akaitwa shujaa wa Mexico.

Akasifiwa sana kwa kiwango kizuri na baada ya kombe vigogo wakaanza kupigana vikumbo wakimtaka, akaamua kwenda zake La Liga kukipiga Malaga na baadaye kwa mkopo Granada, miaka miwili nyavu zake zikaguswa mara 82 na timu ikashuka daraja.

Sajili kama hizi unaweza hisi ndizo ambazo zimemfanya Axel Witsel kuzikimbia klabu kubwa, pamoja na kiwango chake kikubwa ameamua kujichimbia zake Chinaaa akiwa na miaka 27 tu.

Lakini vilabu vikubwa vinapigwa zaidi kipindi hichi kwani mawakala nao wa wachezaji hawa huwa wanautumia muda huu kuchuma pesa kutoka kwenye vilabu ambavyo vinawataka wateja wao.

Achana na Luis Suarez ile ada ya £65m kwenda Barcelona, wengine wanaweza kusema ilitikana na fomu ya Liverpool, lakini ada ile ilichagizwa na kombe la dunia pia.

Keylor Navas kwa mfano, ripoti za TMS(Transfer matching system) zinasema mwaka 2013 alikuwa ana thamani ya $900,000 tu lakini baada ya kombe la dunia mwaka 2014 thamani yake ilipanda hadi kufikia $10m.

Sasa safari hii kuna Yerry Mina ambaye Barca walianza kuonesha kutaka kumuuza lakini kombe la dunia limewafanya kuonekana kuanza kusita sita kumtoa mlinzi huyo aliyeng’ara na Colombia.

Yupo Harry Maguire thamani yake haiwezi kuwa £17m ambayo Leicester walimnunua toka Hull City, yupo Benjamin Pavard, yupo mlinzi mwingine wa kulia Sime Vrsajko wa Croatia na Thomas Meunier wa Ubelgiji wote hawa kwa kipindi hiki sokoni hawagusiki kutokana na viwango vyao Urusi, ila sasa nunua at your own risk.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here