Home Kimataifa Eden Hazard atachezea wapi msimu ujao?

Eden Hazard atachezea wapi msimu ujao?

14739
0
SHARE

Tayari usajili wa Cristiano Ronaldo kwenda Juventus umekamilika, hii ndio ilikuwa habari kubwa sana ya usajili lakini hivi sasa kuna hili la mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard.

Mashabiki wa Chelsea dunia nzima hii ni habari ambayo hawataki kuisikia lakini waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo laja, na lisemwalo ni Eden Hazard anatakiwa Real Madrid na Barcelona.

Mwanzoni Real Madrid walikuwa wakiongoza mbio hizi lakini sasa klabu ya Barcelona imejitokeza katika mbio hizi na habari kutoka ughaibuni zinasema Barcelona hawataki utani katika hili.

Eden Hazard mwenyewe anaonekana yuko katikati, anaonekana kama anataka kuondoka na anaonekana anataka kubaki. Tofauti na Real Madrid ambao walitaka kutoa pesa tu kwa Chelsea, Barca wenyewe wana dili lingine.

Wababe wa La Liga hao wanataka kumtoa nyota wao aliyetoka Borussia Dortmund Osmane Dembele kama sehemu ya dili hilo la kumnasa Hazard aliyekuwa na kiwango cha hali ya juu kombe la dunia.

Kuna tetesi za chini chini ambazo zinasema wakala wa mchezaji huyo amekutana na Barcelona ili kujaribu kuongelea suala la usajili wake kwenda Barcelona.

Lakini ukiacha hayo, wiki hii Hazard alinukuliwa akimsifu kocha aliyepita wa Real Madrid Zinedine Zidane na kusisitiza kwamba “Real Madrid ni ndoto ya kila mtu”

Florentino Perez tayari amempoteza Cr7 na ni wazi kwamba usajili wa Neymar utakuwa mgumu sana hivyo ni wazi kwamba Real Madrid watatumia nguvu kubwa ya pesa kumnasa Hazard kuwa mrithi wa Cr7.

Achana na Madrid achana na Barcelona, kocha mpya wa Chelsea Marizio Sarri amesema kati ya vitu anavihitaji Chelsea ni Eden Hazard na Chelsea wanajipanga kuitolea nje ofa yeyote itakayoletwa, tusubiri kuona vita hii ya mafahari watatu itaishia wapi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here