Home Kimataifa Bei za jezi mpya za United na Chelsea hazishikiki, Arsenal na Spurs...

Bei za jezi mpya za United na Chelsea hazishikiki, Arsenal na Spurs nao balaa

20297
1
SHARE

Unaambiwa jezi mpya ambayo Manchester United wameitambulisha imezua hasira kwa mashabiki wake baada ya bei ya jezi hiyo kuwa juu kupita kawaida.


Kama unaitaka jezi hiyo ni lazima uwe na pesa sii chini ya 541,070, kwa tshirt peke yake inauzwa karibia 320,000 na kama utahitaji kupata full hadi socks itakugharimu kiasi hicho cha laki 450,000+.


Bukta ya timu hiyo inauza pesa ya Kitanzania shilingi 124,000 huku socks za timu zikiuzwa 75,284 na hii ni kwa mujibu wa bei mpya za kampuno inayotengeneza vifaa vya michezo vya klabu hiyo kampuni ya Adidas.


The Blues/Chelsea nao sio kirahisi kama unavyowaza, wenyewe uzi wao ni £195.85 kuipta jezi full ya klabu hiyo ambapo kiasi hicho ni sawa na karibia na 500,000/= kwa bei ya pesa ya madafu.

Wakati mashabiki wa Manchester United na Chelsea wakilia bei za jezi zao. kwa wenzao Arsenal hali ni tofauti na jezi ya klabu hiyo imeendelea kuuzwa kwa bei ya kawaida.


Ukiitaka jezi mpya ya Arsenal unatakiwa uwe na kiasi cha 295,000 tu kwa tshirt na full itakugharimu 464,197/=, kuipata jezi original ya klabu ya Liverpool kwa tshrt tu unapaswa kuwa na sii chini ya 210,000/= hii ni kwa bei ya Liva msimu uliopita.


Tottenham Hotspur nao wametangaza uzi wao mpya kwa ajili ya 2018/2019 na kama unaitaka jezi mpya ya Tottenham Hotspur unatakiwa kuwa na 473,000 kuipata jezi original ya klabu hiyo

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here