Home Kimataifa “Yanayosemekana” yote kuhusu usajili wa Arsenal, Chelsea na United yako hapa

“Yanayosemekana” yote kuhusu usajili wa Arsenal, Chelsea na United yako hapa

17163
0
SHARE

Kona ya Inasemekana iko hapa kukuletea tetesi zoote na yanayosemwa na magazeti pamoja na vyanzo mbali mbali vya usajili kutoka barani Ulaya.

Inasemekana Petr Cech anakaribia kurudi katika klabu ya Chelsea, Chelsea wanataka kufanya mpango huo kama Thibaut Courtois atakwenda Madrid lakini Chelsea hao hao inasemekana wanataka kujaribu kuzuia uhamisho wa mlinda lango Allison inayesemekana anakwenda Liverpool.

Pale Anfiled inasemekana kwamba klabu ya Liverpool imekubali kutoa kiasi cha £66m kwa ajili ya kumnunua mlinda lango wa As Roma Allison ambaye wamekuwa wakimuwinda kwa misimu takribani miwili sasa.

Lakini Ujerumani nako inasemekana klabu ya Borussia Dortmund imekata tamaa kumnunua Mitchy Batshuayi kutoka Chelsea na sasa klabu hiyo imejipanga kutuma ofa Juventus kwa ajili ya kumnunua Mario Mandzukic.

Inasemekana hii ni habari ambayo mashabiki wa Chelsea hawataki kuisikia kwani inasemekana Real Madrid bado imewaganda Eden Hazard na Thibaut Courtois na habari za magazeti ya Hispania hii leo zinadai Madrid wako tayari kuwapa Chelsea kiasi cha £150m kuwanasa nyota hao.

Klabu za Manchester United na Paris St German zimejikuta katika vita ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Tottenham Hotspur Toby Alderweireld ambaye alikuwa na kiwango kizuri na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Inasemekana Real Madrid wameanza chokochoko kwa Manchester United kuhusu Romelu Lukaku, na wanataka kama United wakimtaka Bale baasi Lukaku awe sehemu ya dili hilo.

Na mwisho kwa leo inasemekana bado Manchester United hawajaachana na Ivan Perisic, klabu hiyo inaendela na mchakato wa kumnasa nyota huyo wa Croatia na sasa wanamhitaji yeye pamoja na nyota mwingine wa Croatia Ante Rebic.

Inasemekana klabu ya PSG ina mpango wa kumuongezea mkataba Neymar hadi kufikia kiasi cha €50m kwa mwaka kutoka €35m kwa mwaka ili kujaribu kuzuia ushawishi wa aina yoyote kutoka Real Madrid.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here