Home Kitaifa Jibu la Masoud Djuma kuhusu Yondani kusajiliwa Simba

Jibu la Masoud Djuma kuhusu Yondani kusajiliwa Simba

21909
0
SHARE

Kuna tetesi zinazomhusisha beki wa kutumainiwa Yanga Kelvin Yondani muda wowote atajiunga na klabu ya Simba kwa ajili ya kuitumikia kwenye ligi kuu na mashindano mengine ikiwemo ya kimataifa.

Yondani hajasafiri na Yanga na inaelezwa kila kitu kinakwenda sawa na dili limefikia hatua za mwisho kabisa.

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema karibia asilimia 80 ya wachezaji waliowataka wamewapata, hawezi kusema wamekamilisha usajili kwa sababu kuna baadhi ya wachezaji walikuwa wanawataka lakini hawajawapata.

Kuhusu usajili wa Kelvin Yondani Masoud amesema: “Hapo sina jib” lakini inaashiria kuna vitu vichache bado havijamaliziwa ili Yondani amwage wino Msimbazi.

Leo saa 1:00 usiku Yanga itakuwa kibaruani kupigania pointi tatu dhidi ya Gor Mahia katika mchezo wa kombe la shirikisho Afrika meneja w timu Hafidh Saleh amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo, mechi itachezwa saa 1:00 usiku. Tumejipanga vizuri mwalimu amemaliza mazoezi jana kwenye uwanja wa Kasarani (mechi itachezwa hapo) wachezaji wote wapo sawa tupo tayari kwa mchezo.”

Meneja amekataa kuzungumzia wachezaji ambao hawajasafiri na timu akiwepo Kelvin Yondani.

“Kuna wachezaji wengine wapo Dar es Salaam, waliopo hapa wameahidi watapigana kufa nakupona kupata ushindi kwenye mchezo wa leo.”

“Sitaki kusema lolote kuhusu hilo, ninachoweza kusema ni kuhusu waliokuja huku (Kenya). Waliobaki Dar es Salaam kuna wengine wana majeruhi, wengine wana matatizo ya kifamilia na wengine wana matatizo hilo sitaki kuliweka wazi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here