Home Kitaifa Dismas Ten kakwamisha usajili wa Ngasa, Kaseke Caf?

Dismas Ten kakwamisha usajili wa Ngasa, Kaseke Caf?

10584
0
SHARE

Kumekuwa na taarifa kutoka kwa wapenzi na wanachama wa Yanga kumshutumu ofisa habari wa klabu hiyo Dismas Ten kwamba amekwamisha usajili wa wachezaji watatu (Deus Kaseke, Mrisho Ngasa na Heritie Makambo) kwenda Caf ambao klabu hiyo ingeweza kuwatumia kwenye kombe la shirikisho Afrika.

Dismas amemwambia Prisca Kishamba kilichotokea hadi wachezaji hao wakashindwa kusajiliwa Caf ni wachezaji hao kuchelewa kusaini mikataba pamoja na kutokidhi baadhi ya vigezo.

“Zimekuwepo taarifa za Kaseke kuja Yanganmuda mrefu kidogo kama wiki mbili au tatu zilizopita lakini taratibu zake za usajili zimechelewa kukamilika, amesaini mkataba Jumamosi iliyopita. Ni vipi utatuma taarifa za mchezaji Caf wakati taratibu zake za kusajiliwa zilikuwa hazijakamikika?

“Mbali na mkataba mchezaji anatakiwa kuwa na  documents nyingine (local licence, medical report) kuchelewa wao kusaini mkataba pengine kulichelewesha na mambo mengine kufanyika.

“Kupitia ofisi ya Katibu Mkuu, baada ya kuwepo taarifa za kusajiliwa Deus Kaseke, Mrisho Ngasa na Haritie Makambo tuliandika barua kwenda kwa Katibu Kuu wa TFF kumuomba atusaidie wachezaji hawa wapate local licence haraka ili tuwaingize kwenye mfumo wa Caf.

“Majibu yalikuja kwamba, hawa wachezaji bado hawajasajiliwa maana yake hawapo kwenye mfumo wa usajili wa ndani kwa sababu walikuwa bado hawajatimiza taratibu zinazotakiwa kwa klabu.

“Jumamosi iliyopita ndio walisaini mikataba na baada ya hapo taratibu nyingine zikaanza ili kuhakikisha wanaingia kwenye mfumo wa Caf, bahati mbaya muda ulikuwa umepita (kwa mchezo huu Yanga vs Gor Mahia).

“Mchezaji kama Makambo ni mchezaji wa kimataifa kwa namna yoyote kwenye uhamisho wake system ya usajili inaelekeza ni lazima awe na work permit, residence permit, ITC na medical report ili kukamilisha taratibu zote za kumtambulisha yeye ni mchezaji halali wa Yanga.”

Kwa nini Dismas anatuhumiwa kukwamisha usajili wa wachezaji hao?

“Wiki mbili zilizopita nilikuwa naumwa sana kwa hiyo katika hali yankawaida nisingeweza kufanya jambo lolote na sikufanya jambo lolote. Kwenye taasisi linapotokea jambo huwezi kuwazuia watu kusema kwa hisia zao hasa linapotokea jambo kama hili ambalo lilitakiwa lifanyike lakini halikufanyika.”

“System ya usajili ipo ofisini (kwenye osifisi ya Katibu Mkuu) nisipokuwepo mimi mtu mwingine anaweza kuja nakuendelea. Lakini pia ipo TFF kama ikitokea nimepoteza uhai haimaanishi usajili hautafanyika watu wengine wanaweza kuchukua na kuendelea mambo yakafanyika na TFF ingesimamia lakini hakukuwa na hizo documents ambazo zingewawezesha wao kuendelea.”

“Hakukuwa na sababu ya mimi kukwamisha, hii ni kazi yangu, mimi ni professional naelewa na nafanya kazi yangu kwa misingi ambayo inatakiwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here