Home Kitaifa Deus Kaseke pekee amekidhi vigezo vya usajili Yanga

Deus Kaseke pekee amekidhi vigezo vya usajili Yanga

16158
0
SHARE

Ofisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema mchezaji pekee aliyekidhi vigezo vya usajili ni Deus Kaseke huku Kelvin Yondani na Hassan Kessy wakiwa hawana mikataba na klabu hiyo.

Dismas alizungumza na Prisca Kishamba kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu usajili wa wachezaji wa Yanga.

“Ukiangalia kwenye mfumo wa usajili wa ndani kwa Yanga, mchezaji pekee ambaye amekidhi vitu vyote vinavyotakiwa kuwepo ni Deus Kaseke, tayari usajili wake tumeutuma tunachosubiri ni TFF kuuthibitisha ili apate leseni ya ndani.”

“Wachezaji wengine wote usajili wao bado upo pending kwa sababu baadhi ya documents zao zinakosekana. Hadi sasa nina medical report za wachezaji watatu, (ya Matheo Anthony ina matatizo) inabidi irudishwe kwa daktari ili aweze kuiweka sawa.”

“Medical report zina gharama yake katika kuzitengeneza. Kabla daktari hajaondoka kwenda Kenya aliniambia kuna kipimo ambacho kinakwenda hadi Tsh. 230,000 ukizidisha kwa idadi ya wachezaji tulionao utaona ni kiasi gani cha fedha kina hitajika.”

“Changamoto ipo lakini baada ya daktari kurudi kutoka Kenya atakuja kukamilisha medical report na baadaye usajili uweze kufanyika kwa sababu baadhi ya wachezaji usajili wao upo pending kutokana na baadhi ya vitu kutokamilika.”

“Wapo wachezaji ambao hadi sasa hawana mikataba, Hassan Ramadhani Kessy, Kelvin Yondani hawana mikataba. Jambo jema ni kwamba kamati ya usajili inaendelea kuzungumza nao ili kuweka mambo sawa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here