Home Kitaifa Wachezaji wa kigeni wataidhoofisha Stars

Wachezaji wa kigeni wataidhoofisha Stars

9748
0
SHARE

Kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imepitisha kanuni kuruhusu timu moja kusajili idadi ya wachezaji 10 wa kigeni kucheza ligi kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao.

Wachezaji hao wanaweza kutumika wote kwa pamoja katika mchezo mmoja. Kikao kikao hicho kilifanyika July 12, 2018 makao makuu ya TFF Dar.

Kocha wa Lipuli FC Selemani Matola amesema kuruhusu vilabu kusajili wachezaji 10 na wacheze kwa wakati kutaiathiri timu ya taifa.

“Unapomchukua mchezaji wa kigeni siku zote anatakiwa kuwa na kitu cha ziada na acheze, maana yake kama kuna timu zitaweza kusajili wachezaji 10 wenye vitu vya ziada na wote wakapata nafasi ya kucheza maana yake ni mchezaji mmoja wa kitanzania ndio atapata nafasi ya kucheza kwenye timu hizo”- Selemani Matola.

“Vilabu ambavyo vinaweza kuwa na wachezaji 10 wa kigeni kwa msimu ni Simba, Yanga na Azam lakini vilabu vingine vinauwezo wa kuwa na wachezaji wa kigeni watatu au wawili lakini haviwezi kusajili wachezaji wote 10.”

“Kwa upande wa Simba, Yanga na Azam inaweza kuwa faida kwao kwa sababu wanaweza kuwasaidia kwenye mashindano ya kimataifa lakini athari yake ni kuua timu ya taifa vilabu hivyo (Simba, Yanga na Azam) ndio vinatengeneza timu ya taifa.”

“Vilabu hivi vinaweza kuwahudumia wachezaji vizuri kwa ajili ya mahitaji ya kimpira tofauti na vilabu vya mikoani. Wanaweza kulipa mishahara vizuri, kambi nzuri na mambo mengine lakini kama wachezaji wazawa hawatatumika kwenye vilabu hivi huko mikoani hakuna timu inayoweza kutoa wachezaji wa kutosha wenye ubora kucheza timu ya taifa.”

Watu wanatolea mfano ligi ya Congo DR kwamba ina wachezaji wengi wa kigeni lakini timu yao ya taifa inafanya vizuri, wanasahau Congo wakiita timu ya taifa hawategemei wachezaji wa ndani wachezaji wao wengi wa timu ya taifa wanatoka nje sisi bado tunategemea wachezaji kutoka kwenye ligi yetu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here