Home Makala Mfahamu Mbappe mchezaji tishio zaidi kombe la dunia 2018

Mfahamu Mbappe mchezaji tishio zaidi kombe la dunia 2018

11155
0
SHARE

Katika umri wako wa miaka 19 una nini? au uliwahi kumiliki nini? au una mpango wa kumiliki nini? Hapo baadae utajivunia kipi kwa wanao hapo baadae? Utaelezea kitu gani? Unadhani wewe na Mbappe yupi hadithi yake kwa wanae na wajukuu zake itawavutia zaidi? Kila mtu hapa duniani amezaliwa na bahati yake.

Kylian Mbappé alizaliwa kaskazini mwa Paris kule Bondy umbali wa kilometa 11. Mbappe Lottin alizaliwa miezi sita baada ya tu kombe la dunia kukamilika kule Ufaransa.

Hakukulia kwenye kilimo cha korosho! la hasha! wala hajui jembe ni nini, yeye alikulia kwenye akademi ya soka.

Kylian Mbappé ameisaidia “Les Bleus” kutwaa taji lao ya 2 la dunia. Ameisadia timu yake kupata ushindi wa 4-2 Croatia kule Moscow ndani Luzhniki Stadium na kuwa mabingwa wapya mbele ya mabingwa wa soka duniani Messi na Ronaldo.

Wakati dunia inamjadili kijana huyu mwenye miaka 19 tu, tuna mengi ya kufahamu kutoka kwake. Mbappé aliipatia France ushindi dhidi ya Peru, 1-0, na kumuondosha Leo Messi na Argentina yake kwa kutia kimyani mabao mawili kwenye ushindi wa mabao manne.

Baba yake alikuwa kocha na mchezaji wa klabu ya AS Bondy iliyokuwa chini ya raisi Atmane Airouche. Nyakati hizo ndo kwanza Mbappe aliachishwa maziwa. Raisi huyo anasema Mbappe alikuwa akipenda sana mpira kuliko hata kula.

Baba yake Mbappé bwana Wilfried ni mzaliwa wa Cameroon.

Mwandishi mmoja kutoka Nigeria ajulikane kama Tana Aiyejina nae alikuja na hoja kwamba Mbappe ana asili ya Nigeria na sio Cameroon pekee.

Mama yake Mbappé’s ni mzaliwa wa Algerian na anajulikana kama Fayza Lamari, ambaye iia alicheza mpira wa mkono ligi daraja la kwanza katika klabu ya Bondy miaka ya 1990 mpaka 2000. Hata hivyo mama yake aliwahi kuingia kwenye kasheshe akiwatuhumu sana wachezaji wa PSG akiwataja Neymar, Alves na Silva kumtania mwanae kwa kumtumia vinyago vya ajabu.

Mwezi februari mwaka huu Neymar na Mbappe hawakuwa kwenye mahusiano mazuri mara baada ya taarifa kudai kwamba Mbappe aligoma kwa makusudi kumpa pasi Neymar. Mama yake akadai kuwa utani wanaomfanyia mwanae sio mzuri na hauna tija kwemye nidhamu ya soka bali ni masikhara yasiyo na manufaa kwa mwanae.

Taarifa zinasema kwamba mzee Wilfred Mbappe, alikuwa mkimbizi hapo awali na aliamua kutimkia France kutafuta maisha. Ili kupata uraia wa kudumu kule France ilibidi amuoe mwanamke mzaliwa Algeria mwenye asili ya France Fayza.

Kylian alipewa jina la KiYoruba kabila la huko Nigeria akaitwa Adesanmi maanake “Nafaa kuwa mtawala” Mzee Wilfred, pia alikuwa baba mlezi wa Jirès Kembo Ekoko, mwenye asili ya Congo. Kylian pia ana mdogo wake anayejulikana kama Adeyemi Mbappe,

Adeyemi manake Yoruba ni “uvikwe taji.” Mara nyingi Mbappe anaposhangilia kwa kubana mikono makwapani huwa anafanya hivyo ikiwa ni ishara ambayo mdogo wake hupenda kufanya kila mara wanapocheza michezo ya game, mdogo wake akimfunga huwa anashangilia kwa aina hiyo.

Hapo mwanzoni palikuwepo na fununu kwamba Mbappe huenda akawa mjukuu wa Samuel Mbappe Leppe. Leppe, aliichezea Oryx Douala miaka 1950s na 1960s, akashinda makombe matano ya ligi na vikombe vingine vitatu (1963, 1968 na 1970) Alikuwa nahodha wa kwanza kubeba kombe la African Champions Clubs’ Cup mwaka 1964/65 lakini fununu hizo hazikuwahi kuthibitishwa na upande wowote.

Kaka yao Mbappé , Jirès Kembo-Ekoko anacheza huko uturuki kunako klabu ya Bursaspor, na mdogo wake Ethan, mwenye miaka 12, yupo kwenye kikosi cha U-12 cha Paris Saint-Germain (PSG).

Mashindano mechi Magoli asisti Njano N/R Nye dakika
Jumla : 105 48 33 6 1 6.713′
68 29 20 5 3.959′
17 10 3 1 1.194′
9 6 6 812′
8 3 2 1 613′
1 1 34′
1 1 30′
1 71′
Mwalimu wake wa zamani bwana Antonio Riccardi anasema Mbappé akiwa na miaka 6 tayari alikuwa kiongozi na mchezaji tegemezi wa klabu ya umri wa miaka 10.Alipofikisha umri wa 12, Mbappé alikwenda kufanya maajaribio katika kituo cha kulea vipaji cha Clairefontaine football centre.

Katika umri wa miaka 14, alipata nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha wakubwa cha Monaco. Alifanya hivyo kwa kipindi kirefu kabla hata hajamaliza elimu ya juu ya sekondari. Alicheza mchezo wake wa kwanza kwa Monaco akiwa na umri wa 16 na siku 347 na kuvunja rekodi iliyowekwa hapo awali na Henry, alipokuwa na miaka 17 na siku 14 takribani miaka 20 iliyopita.

Mbappe akiwa na umri wa miaka 18 alifunga mabao 26 kwenye msimu wake wa kwanza pale Monaco. Kwa kiwango kile Real Madrid Waliingia mfukoni kutoa kitita cha £161m kabla ya PSG kumnasa.

Mbappé alipojiunga na PSG aliweka rekodi ya kuwa kijana mchanga zaidi duniani kuwahi kulipwa mshahara mkubwa. Monaco walikubaliana na PSG kuuziana mchezaji huyo kitita cha €180 million (zaidi US$210.4 million) baada ya mkopo wake kukamilika.

Ameweka rekodi kubwa katika fainali za kombe la dunia kwa kuwa kijana mdogo zaido kuwahi kufunga bao katika fainali za kombe la dunia tokea Pele kufanya hivyo mwaka 1958.

Timu ya Taifa
2014 France U17 2 (0)
2016 France U19 11 (7)
2017– France 22 (8)

Tuzo zake Binafsi

Kikosi bora cha UEFA European U-19 Championship : 2016
Chezaji chipukizi wa ligi kuu Ufransa kupitia UNFP Ligue 1 : 2016–17, 2017–18
Kikosi bora cha UNFP Ligue 1: 2016–17, 2017–18
Mchezaji bora wa mwezi kupitia UNFP: April 2017, March 2018
Kikosi bora cha UEFA Champions League : 2016–17
Kikosi bora cha tatu ch FIFPro World XI: 2017
Golden Boy: 2017
Mchezaji bora chipukizi wa kombe la dunia:2018

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here