Home Kimataifa Manchester United wamuacha Alexis Sanchez kutokana na uhalifu

Manchester United wamuacha Alexis Sanchez kutokana na uhalifu

12145
0
SHARE

Tayari wachezaji wa Manchester United ambao hawakuwepo katika michuano ya kombe la dunia pale nchini Urusi wametua Marekani kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Juan Mata, Ander Herrera, Eric Bailly na Anthony Martial ni moja kati ya nyota ambao wameongozana na kikosi hicho kilichoweka kambi mjini Los Angeles.

Lakini katika hali ambayo imewashangaza wengi nyota wa Manchester United Alexis Sanchez hajasafiri na timu licha ya kwamba alionekana akiwa katika mazoezi ya timu hiyo mjini Manchester siku chache zilizopita.

Sanchez amenyimwa Visa ya kwenda nchini Marekani kutokana na taifa hilo kutoruhusu mtu yeyote mwenye makosa ikiwemo ukwepaji wa kodi au anayetumikia adhabu yeyote kuingia katika nchi hiyo kabla adhabu yake haijaisha.

Hii ilisababisha United wamuache nchini Uingereza na wao wakatangulia Marekani huku Sanchez akiwa anashughulikia suala hilo pamoja na mwanasheria wake ili kuona namna gani anaweza kusafiri.

Ikumbukwe Alexis Sanchez bado anatumikia adhabu ya kifungo cha nje ya miezi 16 ambayo aliipewa mwezi February na mahakama ya nchini Hispania baada ya nyota huyo kudaiwa kukwepa kodi akiwa nchini Hispania.

United wanaanza michezo yao ya kujiandaa na msimu mpya wa Epl kwa kucheza mechi ya kwanza Ijumaa dhidi ya Club America ya Mexico lakini pia watacheza na Liverpool, Ac Milan na Real Madrid wakiwa nchini humo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here